Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

FYATU MFYATUZI: Fyatu kuwafyatua wateule wajigongao na kujikomba



Wanatumia vitegemezi, washirika wa bedroom kunivisha kiremba cha ukoka. wanaboronga halafu wanajigonga na kujikomba kwangu ili waendelee kunigeuza bunga.

Huwa sipendi sifa. Mie ni Fyatu. Siyo Mungu wala muungu. Wafuatao wajiandae kufyatuliwa wote: Mosi, Wapo matapeli na mazwazwa wanaowatumia ndugu zao hata vitegemezi vyao ambvyo bado vimevaa dipers kisiasa kujigonga na kujipendekeza kwangu wasijue sipendi kamchezo haka ka kitapeli na kifwala.

Sitaki kukwezwa wala kupewa sifa nisizo kuwa nazo. Unakuta jitu zembe hata kufikiri eti nalo linataka kuniingiza cha kike kwa kunipa sifa za kipuuzi.

Mtanisifu nikiachia ngazi a uni kugeuza bunga na zwazwa kama nyinyi? Mkome na kukomaa kabla hamjakomolewa. Juzi, niliona kitetemezi cha zwazwa moja nene mtandaoni eti likinisifu kwa kumpa ulaji dingi wake!

Acheni vitegemezi visome na kujitegemea na siyo kutegemea majina ya ukoo. Eti linanisifia na kunipongeza kwa ajili ya dingi wake.

Komeni huu mchezo ambao ni balaa kwa kaya kesho msipoangalia. Msiendekeze njaa na uzwazwa kana kwamba hakuna kesho.

Pili, mafisadi, mafisi, na majambazi ya kisiasa wenye makandokando yanayonuka na kuwaumiza mafyatu tena kwa kupiga njuluku yao ndefu.

Utakuta Fyatu linanuka uchafu wa kila aina yajapo maadili halafu eti linanisifia ili nifumbie macho uchafu na ukatili wao kwa Mafyatu wangu walio wengi.

Mmenoa na mtaishia kuula wa chuya.  Hii mjizi na mijambazi inayonisifusifu inadhani sijui mazabe yake.

Nayaona mengi kwenye mitandao ya kijamii yakijikomba kwangu ili niyape uteuzi. Mengi utakuta ni mifyatu iliyokwisha retire na kuexpire ukiachia ile mivivu ya kufikiri iliyokosa ubunifu ikashikilia umdudu,ushamba, na uzwazwa. Japo nimekuwa najifanya siyanyaki haya machezo, nayanyaka na kuyanyamazia kwa muda.

Acbeni ujambazi na wizi na siyo kujificha kwenye kunisifiasifia. Sisifiki wala sipendi sifa kama wale wapenda sifa uchwara. Hamjui kuwa kupenda sifa ni aina fulani ya ugonjwa wa akili na utumwa licha ya kuwa uzwazwa?

Tatu, wenye shahada, vyeti feki na za kununua au kuzawadiwa kimchongomchongo. Hawa nina maya nao hakuna mfano. Unakuta jitu liliogopa umande halafu linanunua PhD na kuanza kujiita daktari. Mnaujua ugumu wa kuupata huo udaktari au ni uzwazwa unawasumbua? PhD siyo ya kila mmoja bali wachache kama mie Fyatu Mfyatuzi ambaye ninazo magunia tena za kusotea siyo kununua au kupewa.

Nne, wanaopenda eti kuniombea. Mnaiombia kwani mie maiti hadi niombewe au mnajiombea kwa kujifanya mnaniombea? Hapa haombewi Fyatu. Kama kuomba, najiombea mwenyewe.

Siko tayari kuombewa na mifyatu yenye midhambi inayonuka hakuna mfano. Kama kuomba dili, basi jiombeeni kwanza niache kuwapiga na kuwahangaisha nyambaff wakubwa nyie. Utakuta haya yenye magunia ya madhambi yanayojitia kuniombea yanatenda dhambi kila uchao. Yapo mauza mihadarati, mazinzi, maongo, mafitini na kila balaa halafu eti yananiombea. Mnadhani Sir God ni zwazwa kama nyinyi? Mkome kabla sijawaombea muungue mkiwa hai.

Tano, wapendao kunipogeza hata kwa upuuzi. Mbali na kusifiwa, napongezwa hata nikipiga chafya. Haya mazwazwa yanifanya niwe na uwezo wa ajabu.

Yananifanya tajiri kuliko hata Ilon Musk yule mbaguzi wa kwa mzee Madiba aliyeukata kule kwa Joji Kichaka. Lisrikal langu likitimiza wajibu wake kama vile kutoa huduma za kijamii, nasifiwa mimi kana kwamba njuluku inayotumika ni yangu. Utayasikia yakisema “Mheshimiwa Mpendwa na Msikivu sana Fyatu amefanya hili au lile.” Komeni. Natumia njuluku za Mafyatu ambazo nyingine nazipiga, sorry, nazitunza.

Sita, wanaonizeesha kwa kuniita dingi yao. Fyatu ni dingi wa vitegemezi vyetu na bibi Mkubwa siyo dingi wa wote. Kama hamuwajui madingi zenu, nendeni kaulize waliowazaa wawambie kuliko kunipakazia uzinzi wa kuzalisha kila jikombaji, tapeli, na zwazwa.  Kama ilivyo kwenye sifa za kipuuzi, nikachia ulaji mtaendelea kuniita dingi wenu? Unafiki na utapeli mtupu. Kwani, mnanifanya mie hamnazo au kipofu ambaye siwezi kujua wala kuona wengi wa wanaoniita dingi wao ni wazee kuliko mimi? Niliwazaaje wakati walizaliwa kabla sijazaliwa? Kama kuwa dingi wa kila Fyatu ni dili basi, kawatafute wapenda sifa majuha na mazwazwa muwaite dingi zenu. Nimechoka na sifa hizi za kikumbaff.

Sasa nimalizie. Nawashauri wote wanaofanya hayo hapo juu wajue:

Mosi, siyapendi wala kuyahitaji hayo machukizo na usanii wanavyofanya kwa namna yoyote.

Pili, hayatawasaidia kwa vile hawatafanikiwa kuniingiza mkenge kizwazwa hivi. Hivyo, wakome kabisa.

Tatu, najua kila machezo yote. Hivyo, wasiendelee kufanya hayo. Kwangu, hayatawasaidia zaidi ya kuwaumiza.

Kama wana ugonjwa wa kuyafanya hayo, nawashauri wakawatafute wasiowajua na wanaoyapenda tokana na kukosa sifa na kutojiamini. Mie ni bonge la msomi tena profesa wa kweli.

Nne, mimi siyo Mungu wala muungu bali Fyatu wa kawaida mwenye udhu hakuna duniani. Hivi wakijua ukweli kuwa huwa nafaidi sifa watanifanya nini? Kumbe bangi!!