Hoja za Lema kusikilizwa Desemba 28

Friday December 23 2016
LEMA

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema

Arusha. Rufaa ya kupinga kunyimwa dhamana Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema imepangwa kusikilizwa Desemba 28 mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, Salma Maghimbi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa jana, wakili wa Lema, Sheck Mfinanga alisema wamewasilisha hoja sita ndani ya rufaa hiyo.

Alisema katika rufaa hiyo wanapinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha kumnyima dhamana mbunge huyo. Wakili huyo alisema tayari rufaa hiyo imepokewa mbele ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha na kusajiliwa kwa kupewa namba 126.

Habari zaidi soma Gazeti Mwananchi

Advertisement