Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lema azuiwa kutoka nchini, Uhamiaji waeleza sababu

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Godbless Lema.

Muktasari:

  • Safari ya mwanasiasa, Godbless Lema kwenda jijini Nairobi nchini Kenya, imeota mbawa, baada ya kudaiwa kuzuiwa katika mpaka wa Namanga.

Dar es Salaam. Mwanasiasa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Godbless Lema amezuiwa katika mpaka wa Namanga alikokuwa anafanya taratibu za kusafiri kwenda Nairobi nchini Kenya.

Kwa mujibu wa Lema, safari yake kwenda jijini humo, ni kwa ajili ya kufanya matibabu ya maradhi yanayomsumbua, lakini alipofika mpakani akaambiwa hawezi kusafiri.

Hata hivyo, ilielezwa kuwa saa tatu baadaye, hati yake ya kusafiria ilishikiliwa na Idara ya Uhamiaji na akaelekezwa kurejea nyumbani kwake.

Tukio la Lema, linakuja wiki tatu baada ya kiongozi mwingine wa chama hicho, Amani Golugwa azuiwe kusafiri kwenda Brussels nchini Ubelgiji, kuhudhuria mkutano wa Shirika la Umoja wa Demokrasia Duniani (IDU) katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi, kukamatwa kwa Golugwa ni kutokana na tabia yake ya kuingia na kutoka nchini mara kwa mara bila kufuata taratibu za kisheria.

Idara ya Uhamiaji kupitia Msemaji Mkuu, Paul Mselle imekiri kuzuiwa kwa Lema pamoja na hati yake ya kusafiria kushikiliwa. Pia, imesema mwanasiasa huyo anatakiwa kuripoti katika ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji kwa mahojiano zaidi. 

Msele katika taarifa yake iliyotollewa leo Ijumaa Juni 6, 2025 imesema utaratibu huo ni wa kawaida na kwamba, unaweza kufanyika kwa yeyote iwepo Idara hiyo inahitaji kumfanyia mahojiano.
Alipotafutwa kuzungumza kwa kina kuhusu hilo leo, Ijumaa Juni 6, 2025, Lema amedai alifika Namanga saa 6:30 mchana na kuanza michakato ya kumwezesha kusafiri kwenda nchini Kenya kwa ajili ya matibabu.

Baada ya kuonyesha hati ya kusafiria, amesema alitakiwa kufanyiwa ukaguzi wa sura na alama za vidole, ndipo alipoambiwa kuwa yeye ni miongoni mwa walio katika orodha ya wasiotakiwa kusafiri kwenda nje.

“Wakanambia wanaomba wanipeleke katika ofisi ya kiongozi wao wa eneo lile, nikaletwa hapa ofisini na naambiwa wanasubiri maelekezo kutoka kwa viongozi. Bado niko hapa (ilikuwa saa 8:50),” amesema.

Amesema hajafahamu kwamba ni muda gani ataruhusiwa kusafiri, kwa sababu waliomzuia wamemwambia wanasubiri maelekezo kutoka kwa viongozi wao.

Awali, kabla ya kuzungumza na Mwananchi, Lema aliandika katika ukurasa wake wa X, akisema alifika mpakani hapo kwa ajili ya safari kwenda Nairobi.

Alipokuwa anafanya utaratibu wa safari, aliambiwa kuna zuio la viongozi wa Chadema kusafiri kwenda nje ya Tanzania.

“Niko katika ofisi za uhamiaji nasubiri maelekezo kutoka juu, wasiwasi ni mkubwa sana na mashaka, siku moja haya mambo yatakwisha kabisa,” ameandika Lema.
Hata hivyo, Idara ya Uhamiaji imewataka wananchi kupuuza madai hayo akisema utaratibu huo ni wa kawaida na kamwe hauwalengi viongozi wa Chadema bali ni mtu yeyote.

Baadaye, Mbunge huyo wa zamani wa Arusha Mjini, aliandika tena katika ukurasa wake huo, akidai amezuiwa rasmi na hati yake kusafiria imechukuliwa.

“Hati yangu imechukuliwa na sasa napaswa kurudi nyumbani Arusha. Kwa maelezo zaidi niende Makao Makuu ya Uhamiaji Dodoma. Maumivu niliyonayo ni makali sana, nilipaswa kutazama upya afya yangu zaidi kesho Nairobi, sasa siwezi tena kuendelea na safari,” amesema.

Amedai anaamini hicho alichokiita mateso na wasiwasi vitaisha na kamwe havitaendelea kwa vizazi vijavyo.

“Hata watoto wa watesi wetu hawapaswi kuishi pia kuishi hivi. Nilitaka kuwachukia uhamiaji lakini nafikiri hawana kosa lolote. Huu wito nimeuchagua ni mgumu sana kwangu na familia yangu. Yatapita,” amesema.

Alipoulizwa alijuaje iwapo kuna madai ya kuwepo zuio la viongozi wa chama hicho kusafiri nje ya Tanzania, Lema amejibu aliambiwa na Kaimu Naibu Katibu Mkuu Bara, Amani Golugwa.

Kwa mujibu wa Lema, Golugwa alidai kuzipata taarifa hizo baada ya kuzuiwa kwenda nchini Ubelgiji.

Mei 13, mwaka huu, Golugwa alizuiwa na kushikiliwa na Jeshi la Polisi katika Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam, alikokuwa akifanya taratibu za kusafiri kwenda nchini Ubelgiji kushiriki mkutano wa IDU.

Taarifa ya jeshi hilo, ilikiri kumshikilia kwa tuhuma za kusafiri kwa siri kwenda na kurudi nje ya Tanzania.


Chadema yatoa neno

Katika taarifa yake kwa umma, iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi, Benda Rupia imetoa wito kwa mamlaka husika kumrudishia Lema hati yake ya kusafiria, pia imruhusu kuendelea na safari