Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msigwa awaomba radhi wananchi Iringa, awaahidi kuingo’a CCM

Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa.

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa Msigwa, wananchi hao ndio waliomweka katika ramani za siasa, akisema alikimbia vita katikati ya matatizo na hakupaswa kukikifanya kile alichokifanya bali alitakiwa kuangalia kwa picha kubwa ya kutetea haki za wanyonge.

Dar es Salaam. Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa amewaomba radhi wananchi wa Iringa kwa kitendo chake kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM), mwaka jana.

Kwa mujibu wa Msigwa, wananchi hao ndio waliomweka katika ramani za siasa, akisema alikimbia vita katikati ya matatizo na hakupaswa kukikifanya kile alichokifanya bali alitakiwa kuangalia kwa picha kubwa ya kutetea haki za wanyonge.

Baada ya kudumu CCM kwa zaidi ya mwaka mmoja, Mei 23, 2026 Mchungaji Peter Msigwa alirejea katika chama chake cha zamani cha Chadema na kupokewa na kukabidhiwa kadi ya uanachama.

Msigwa ameomba msamaha huo leo Jumamosi Juni 13, 2026 katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa, ulioudhuriwa na Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, John Heche.

“Picha kubwa kuwa na sauti kwa watu wasiokuwa na sauti, sina maneno mazuri sana, naomba mniwie radhi. Hakuna maisha magumu kama kuishi kwa wakwe (akiwa CCM), nilikuwa ukweni,” amesema Msigwa.

Mchungaji Msigwa aliyehudumu Jimbo la Iringa Mjini kwa miaka 10 amesema katika biblia Yesu alikuwa na wanafunzi 12, kati yao wawili waliteleza kama yeye.

“Naomba mnisamehe nilijali zaidi 'ego' yangu sikuangalia picha pana, niwaahidi mbele yenyu nitakuwa kama simba aliyepoteza watoto wake kuing’oa CCM,” amesema.

“Wangapi mmenisamehe? Akajibiwa wote na wanachama waliohudhuria mkutano huo,” amesema Mchungaji Msigwa.

Katika hatua nyingine, Msigwa ambaye ni mjumbe wa zamani wa kamati kuu ya chama hicho, amesema aliimisi’ (kuikumbuka) kauli mbiu ya chama hicho ya Peoples’ Power wakati alipokuwa CCM.