Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Faye wa Senegal aanzisha chama chake

Rais wa Senegal, Bassirou Faye

Muktasari:

  • Hatua hiyo, inakuja baada ya mkuu huyo wa Taifa ya Senegal kuingia katika mgogoro na kiongozi wa chama tawala kilichompa urais.

Senegal. Rais wa Senegal, Bassirou Faye, ameanzisha rasmi chama kipya cha kisiasa, hatua inayothibitisha kuvunjika kwa ushirikiano wake wa kisiasa na kiongozi wa chama tawala cha Pastef, Ousmane Sonko.

Chama hicho kipya kinachoitwa Republican Patriots, kilizinduliwa jana Jumamosi Julai 26, 2026 baada ya miezi kadhaa ya mvutano kati ya Faye na Sonko, ambaye ndiye kiongozi wa chama cha Pastef, kilichompa urais Faye.

Faye na Sonko walishinda uchaguzi wa urais wa mwaka 2024 kwa pamoja, wakiahidi kupambana na rushwa, kuongeza ajira na kusimamia rasilimali za mafuta, gesi na madini.

Hata hivyo, uhusiano wao ulianza kudhoofika kutokana na tofauti kuhusu sera muhimu za serikali, hasa namna Senegal inavyopaswa kushughulikia mazungumzo na Shirika la Fedha Duniani (IMF).

Mvutano huo uliongezeka baada ya Faye kumuondoa Sonko katika nafasi ya waziri mkuu na kumteua Ahmadou Al Aminou Lo kuchukua nafasi hiyo.

Licha ya kuondolewa kwake, Sonko aliendelea kuwa na ushawishi mkubwa baada ya chama chake cha Pastef kubaki na wabunge wengi na kuchaguliwa kuwa spika wa bunge.

Baadhi ya viongozi wakuu wa Pastef, viongozi wa mikoa na wanachama vijana wa chama hicho wameanza kuhamia kwenye chama kipya cha Faye.

Pia, baadhi ya wanasiasa kutoka chama cha upinzani cha Alliance for the Republic wamejiunga na kambi ya Rais Faye, kuongeza nguvu kwa chama chake kipya.

Juni mwaka huu, baraza jipya la mawaziri lililoundwa halikuwa na viongozi wa Pastef baada ya Sonko kutangaza chama chake hakitashiriki katika serikali.

Mgawanyiko huo, umeibua wasiwasi kuhusu mustakabali wa ajenda ya mageuzi iliyowapeleka madarakani viongozi hao wawili.

Serikali ya Faye, imekabiliwa na shinikizo la kiuchumi baada ya kubaini kuwa utawala uliopita ulificha kiwango halisi cha mikopo ya taifa.

Taarifa hizo, zimeongeza mzigo wa deni la Senegal na kufanya utekelezaji wa ahadi walizozitoa kwenye kampeni kuwa changamoto.