Ulanguzi tiketi wazoa watu 10 Ubungo

Friday December 23 2016
pic ubungo

Tumaini Msowoya, Mwananchi

[email protected]

Dar es Salaam. Wakati sherehe za mwisho wa mwaka zikianza kesho, zaidi ya watu 10 wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuwatoza nauli kubwa abiria katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Ubungo.

Habari zilizopatikana kituoni hapo jana, zilisema watu hao walikuwa wakiwatoza abiria nauli tofauti na iliyopangwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra). Pia, zaidi ya mabasi sita yalizuiwa kufanya safari zake baada ya ukaguzi uliofanywa na askari wa usalama barabara kubaini yana hitilafu.

Mwananchi ilishuhudia umati mkubwa wa abiria wanaosafiri huku kukiwa hakuna mabasi ya kutosha ya kuwasafirisha hali inayowafanya baadhi yao kulanguliwa nauli.

Habari kamili soma Gazeti Mwananchi

Advertisement
Advertisement