Vipaumbele vya mwenyekiti mpya wazazi CCM hivi hapa

Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Fadhil Maganya akiwashukuru wajumbe wa mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo kwa kumchagua. Picha Ramadhan Hassan

Muktasari:

Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM), Fadhil Maganya ametaja vipaumbele vinne atakavyoanza navyo.

Dodoma. Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM), Fadhil Maganya ametaja vipaumbele vinne atakavyoanza navyo.

  

Maganya ametaja vipaumbele vyake baada ya kushinda nafasi hiyo vikiwamo ujenzi wa hospitali kubwa ya Rufaa, Wazazi Commecial Bank, Mfuko wa wazazi na ufugaji wa kisasa.


Maganya aliibuka kidedea katika uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi uliofanyika jana Alhamisi jijini Dodoma na kupata kura 578 kati ya 835 akiwashinda wagombea wengine saba akiwemo mwenyekiti waliyepita Dk Edmund Mndolwa.


Mwenyekiti huyo amesema anataka Jumuiya hiyo iwe na Hospitali kubwa ya rufaa ambayo itatoa tiba kwa Watanzania.


"Nataka tuwe na Wazazi Commercial Bank, Wakfu kwa wazazi kazi yake itakuwa ni kushawishi misaada uwezo ninao maarifa ninayo tunaenda kutekeleza haya," amesema Mwenyekiti huyo.


Pia, amesema kipaumbele chake kingine ni ufugaji wa kisasa ambao utaibadilisha kiuchumi Jumuiya.


"Ninajua watumishi zipo kero mbalimbali sioni sababu nitashirikiana na Katibu Mkuu tuweze kuziweka wazi zinatatulika tu,"amesema Mwenyekiti huyo.