Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KONA YA WASTAAFU: Ili kuboresha maisha ya mstaafu!

Kuna mambo mengine unapoyasikia siri- kali na kibubu kinachotunza na kufanyia biashara kwa akiba yetu vikijinasibu kwamba vinayafanya ili kuboresha maisha ya mstaafu aliyeijenga nchi hii, unaishia kucheka uchungu, sijui kama hata kicheko chenyewe kitatoka!

Utaishia kucheka kwa uchungu,  siri-kali inapodai kuwa inaboresha hali ngumu ya maisha inayomkabili mstaafu, kwa kumuongeza Sh50,000  kwa mwezi kwenye pensheni yake ya Sh105,000 anayopata kwa mwezi kwa miaka 21. Sh50,000! Yaani mstaafu upate pensheni ya Sh105,000 kwa mwezi kwa miaka 21, halafu baada ya kuomba na kuomboleza sana siri- kali ikubali kumuongeza sio laki moja au mbili ili apate pensheni ya laki tatu kwa mwezi inamuongeza elfu hamsini, rudia hapo, inamuongeza Sh50,000 ili Sh105,000 ili kuboresha maisha yake!

Huku ni kuboresha kasi ya safari ya mstaafu kwenda Kinondoni !

Kuna njia tatu muhimu za kuboresha, kweli hali ngumu ya maisha inayomkabili mstaafu wa kima cha chini ambazo siri-kali na kibubu kinachotunza hela zake zingepaswa kuzichukua haraka kuboresha kweli maisha ya mstaafu aliyeijenga na kulinda nchi hii kwa jasho na damu.

Njia ya kwanza, ni wastaafu kupandishwa haraka pensheni yao kuwa Sh300,000 kwa mwezi.

Hili halina mjadala, ni jambo linalopaswa kufanywa kwa dharura na linawezekana. 

Waheshimiwa wanaweza wasishtuke, kama ambavyo hawakushtuka kwa miaka 21,  wakisema wastaafu wenyewe wa kima cha chini wamebaki wangapi, bila kukumbuka kuwa idadi yao inaweza kumfanya mtu ausikie ubunge au uheshimiwa wake redioni!

Hili linaweza kuihusu siri- kali na kibubu cha akiba ya mstaafu, kwa pamoja. Siri-kali kwa vile wastaafu wa kima cha chini ndio walioijenga kweli nchi hii kwa jasho na damu mpaka kufikia hapa, wanaosemekana kuwa ni wawakilishi wa wananchi kufikia kulipwa shilingi...mama wee...milioni 14 kwa mwezi huku aliyeijenga nchi mwenyewe akiishia kuboreshewa maisha kwa Sh150,000 mwezi !Aibu naona mimi mstaafu.

Kibubu kinahusika zaidi   katika hili kwa vile kimetunza hela za mstaafu kwa miaka 40 ya ajira yake na kimejiongeza na kufanyia biashara akiba ya mstaafu kwa kujenga magorofa sehemu mbali mbali nchini lakini kodi inayotozwa kwenye maghorofa hayo mstaafu anaishia kusikia harufu yake tu! Haijaelezwa kwa nini mstaafu asilipwe sehemu ya kodi ya ghorofa lililojengwa kwa hela yake, japo mara moja kila mwaka!

Ndio, kibubu kimefanya jambo jema kwa kujiongeza na kutoa Sh5,500,00 kwa wategemezi wa mstaafu pale mstaafu anapokuwa mkazi wa kinondoni.

Sawa, ni jambo jema, lakini mstaafu anadhani ni  jambo jema zaidi kwa kibubu kutoa Sh5,000,000 kumpa mstaafu, akiwa hai, rudia hapo,  akiwa hai,  kisha kutoa hizo laki tano za gharama za kumpeleka Kinndoni!

Tatu, kuanzia Bunge lijalo, Januari mwakani, siri-kali ifanye mshahara wa wabunge uwe Sh5,000,000 kwa mwezi, halafu zile Sh9,000,000 zinazookolewa zigawanywe ili kila mstaafu wa kima cha chini hatimaye  apate pensheni ya Sh500,000 kwa mwezi! Inawezekana, ni utashi tu unaohitajika.

Hii pia itasaidia sana kudhibiti wataalamu wa Taifa na kila anayejua kusoma na kuandika tu kuacha kazi zao muhimu za kujenga Taifa letu na kukimbilia kwenye mshahara wa Sh14,000,000 kwa mwezi !

Mstaafu wetu anaamini kuwa, haya yakifanyika, miaka ijayo itakuwa na idadi ndogo sana ya watangaza nia na mstaafu atakuwa anapokea pensheni ya Sh500,000 kwa mwezi huku akiwa na Sh5,000,000 mfukoni! Inawezekana.

Ni utashi tu, tufanye ili kila mtu apate kipande cha keki ya Taifa, asiishie kusikia harufu tu.


 0754 340606 / 0784 340606