Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Masilahi ya maprodyuza hayataimarika bila mfumo mpya

Muktasari:

Ni vigumu kusema hivyo na ukaeleweka na jamii ya wasanii na maelfu ya mashabiki wao. Lakini huo ndiyo ukweli, iwapo hali ya masilahi inayolegalega katika studio mbalimbali nchini haitaimarika.

Kuna kila dalili kazi ya uzalishaji wa muziki wa Bongo Fleva itapotea au kupoteza thamani miaka michache ijayo.

Ni vigumu kusema hivyo na ukaeleweka na jamii ya wasanii na maelfu ya mashabiki wao. Lakini huo ndiyo ukweli, iwapo hali ya masilahi inayolegalega katika studio mbalimbali nchini haitaimarika.

Kwa nyakati tofauti baadhi ya wazalishaji wa muziki wa Bongo Fleva nchini wamekuwa wakilalamikia tabia ya mastaa wa muziki huo kutumia fedha kidogo kurekodi nyimbo, huku wakitumia mamilioni kurekodi video nje ya nchi.

Mzalishaji mkongwe nchini Master J hivi karibuni alinukuliwa na tovuti ya Bongo 5 akilalamikia aina hiyo mpya ya ‘unyonyaji’. Master J alisema ni dhambi na hakuna kitu kinachouma kama kumrekodia msanii wimbo kwa bei ndogo ya Sh200, 000 baadaye akaenda kurekodi video yake kwa Sh25 milioni Afrika Kusini.

Kulalamika kwa ‘prodyuza’ huyo kumenifanya nipate hofu juu ya hatima ya uzalishaji na ubora wa mziki huo siku zijazo. Habari nyingine kuwa watayarishaji nchini ni maskini kuliko wasanii ni ishara tosha kuwa kazi hiyo inapoteza thamani na imeingiliwa na mamluki.

Pia, inasikitisha kusikia Marco Chali amevunjika moyo kutokana na ‘unyonyaji’ huo na ameacha kufanya kazi. Hii inazidi kuleta wasiwasi katika tasnia ambayo imekuwa kitambulisho muhimu cha Tanzania baada ya Mlima Kilimanjaro, Serengeti na Zanzibar. Sote tunafahamu kuwa hakuna Bongo Fleva au video ya wimbo pasina maprodyuza, lakini kwa nini masilahi kidogo wakati wao ndiyo wakunga? Ili kufahamu sababu za msingi lazima tuangalie asili na mfumo wa biashara ya Bongo Fleva tangu miaka 1990.

Kuna tatizo kubwa la kimfumo wa biashara katika tasnia hiyo ambalo linaikumba pia tasnia ya filamu, Bongo Movie, kwa sasa.

Wakati Bongo Fleva inaanza miaka ya 1990 na mwanzoni mwa 2000 kushika, ilikuwa ni shida kwa msanii kupata studio na kurekodi wimbo wake. Mfumo wa biashara ulikuwa unatawaliwa na studio chache tu kama Bongo Records, MJ Records, Sound crafters au kwa Mika Mwamba.

Wazalishaji wa studio hizo akina Master J, P Funk, Enrico na wengineo walisujudiwa na heshima yao ilionekana. Kibiashara huo ndiyo ulikuwa muda muafaka wa kuujenga mfumo madhubuti wa biashara ya Bongo Fleva.

Hata hivyo, Watayarishaji wengi walibaki wakifanya huruma za kukuza wasanii chipukizi. Asilimia kubwa ya chipukizi na mastaa walibaki katika lebo husika wakitengeneza albamu zao.

Mfumo huo ulitengeneza ‘watoto’ wa studio badala ya wateja ambao wangelipa fedha inayotakiwa kwa huduma stahiki. Tuliwaona akina Juma Nature, Marehemu Mangwair, Jay Moe wakikulia chini ya Bongo Records na kuwa familia.

Mfumo wa aina hiyo ulitengeneza biashara ya ujamaa zaidi badala ya ubepari. Biashara inalipa ukiifanya kiliberali na si kwa kuoneana huruma na kubebana hata kama msanii kipaji kimeshuka au kafilisika.

Lebo kubwa ulimwenguni kama Sony Music, Universal Music, Arista Records na nyinginezo zilitumia mfumo huo lakini mziki wao ulishakua katika misingi ya kibepari. Mwanamziki akiwa anafanya vizuri na kuingiza mapato, anabaki. Aliyeridhika na kushindwa kufanya kazi anatolewa. Msanii naye akiona ananyonywa, ruksa kuondoka.

Mfumo wa kijamaa studio za Tanzania ulisababisha bei za utayarishaji mziki zishindwe kuendana na hali ya soko: mwenendo wa mahitaji na ubora. Ilikuwa ni rahisi kujua upandaji wa mahitaji lakini vigumu kuhakikisha uandaaji unaingiza fedha kupitia ongezeko la wasanii kwa sababu wengi waliendelea kuwa ‘watoto’ wa studio hata baada ya kurekodi albamu.

Dausen ni mwandishi wa Mwananchi. Anapatikana kupitia Twitter @nuzulack