Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mstaafu anapoishia kuwa jiwe kuu la pembeni...

Mstaafu wetu sasa anafikishwa mahali pa kuamini kuwa, kuna Watanzania wachache wanaoonesha wana mawazo mema na muhimu  ya kumjali mstaafu wa Taifa na kumuwezesha kukabiliana kweli na hali ngumu ya uchumi.

Mstaafu wetu amekuwa akisoma jumbe za watu wema kadhaa wanazoandika hapo chini kwenye ukurasa wetu zikieleza jinsi watenda wema hao wanavyoona huruma kwa jinsi hali ngumu ya maisha inayowapata wastaafu wetu wa Taifa baada kustaafu' huku siri-kali ikijinasibu 'kuwawezesha' wastaafu hao, kwa maneno tu bila vitendo, inasikitisha.

Wengi wameishauri na kuitaka siri-kali kuwapa wastaafu' wetu wa kima cha chini wa Taifa kiwango cha pensheni kinachoendana na hali ngumu ya uchumi  inayowakabili, huku siri-kali yetu ikiishia kutoliona, kulijua ama kulidharau tu hilo na ndio maana tunaishia kumuona mstaafu wetu wa kima cha chini akilipwa pensheni ya Sh110,000  tu kwa mwezi kwa miaka 21 sasa, hali ambayo sasa inakuwa kama 'mauaji ya kimbari' kwa wastaafu' hao!

Wasamaria wema hawa wamekuwa wakiishauri na kuitaka siri- kali yetu kufanya mambo muhimu kadhaa ya kuwasaidia kweli wastaafu' wetu wa kima cha chini wa Taifa ambao sasa wamekuwa wa chini kweli, maana hata waajiriwa wa kima cha chini cha mshahara wa sasa wameongezwa mshahara na kuwa Sh500,000  kwa mwezi!

Mshahara huu ni zaidi ya mara nne ya pensheni ya mstaafu  wa zamani wa kima cha chini anayepokea Sh110,000 kwa mwezi kwa miaka 21 iliyopita na nyongeza yake ya Sh50,000 kupata 'wajanja' badala a wastaafu' wenyewe! inashangaza mno kwamba siri-kali haiioni tofauti kubwa hii ya kutisha!

Watu wema hawa wameandika jumbe za kuitaka siri-kali kufanya utaratibu wa matibabu ya bure kwa wastaafu', wameitaka pia siri-kali kufanya utaratibu wa kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa wastaafu' badala ya kuwaacha wakibamizwa na hizi benki za kileo ambazo riba zake hazitofautishi kati ya mstaafu na mfanyabiashara, bali wote ni wakopaji tu ambao hubamizwa na aina moja ya tozo!

Mstaafu wetu anawashukutu sana raia wema hawa wanaotumia muda wao muhimu kuandika jumbe zao fupi hapa kuikumbusha siri -kali inavyopaswa kufanya ili  kuwasaidia kweli wastaafu' wake wa kima cha chini.

Mstaafu wetu anajikuta akitamani kuwa laiti waandikaji meseji hawa wangekuwa kwenye nafasi zenye uwezo na wakafanyia kazi maandishi yao wanayoandika hapa, hakika wastaafu' tungekuwa peponi, bila kulazimika kupitia  Kinondoni kwanza !

Mstaafu wetu wa kima cha chini anaishia kujiuliza kwani yeye amekosa nini hadi ameishia kuwa 'mwanambuzi ambaye kamba ni yake! Anaona waheshimiwa waliokaa kwenye meza huku wakipulizwa na 'kiwinta'  wakifanyia kazi mafaili ya kuendeleza nchi, wanapostaafu wanapata haki ya kupewa gari jipya la bei mbaya linalogharamiwa na siri-kali  kila baada ya miaka miwili mitatu!

Ila yeye wa kima cha chini alitoka jasho la damu juani, akichimba mtaro wa kujenga choo au kumwaga zege ili kujenga maofisi mengi tu anapostaafu hata nyongeza ya pensheni yake inakuwa hadithi au koteshwa mbawa kwenda kushughulikia  mambo yanayoonekana muhimu zaidi kuliko uhai wa mstaafu wa kima cha chini!

Mstaafu anauliza, hivi hii ni nchi aliyoijenga mwenyewe au ilijengwa na waheshimiwa tu?

Mstaafu wa kima cha chini wa Taifa amekosa nini, huku wastaafu wenzake aliojenga nao nchi sasa wanabadilishiwa magari ya bei mbaya, licha ya kupewa nyongeza ya pensheni kila baada ya miaka miwili mitatu, huku yeye  akiishi na pensheni ya 'laki si pesa' kwa mwezi kwa miaka 21 na hatimaye tunapopata nyongeza ya Sh50,000  inaishia kwenye vyombo vya habari tu na kuishia kupigwa kabali?

Ni mambo kama haya ndio humfanya mstaafu wetu kukumbuka sana filamu ya hollywood ya mwaka 2007 iliyochezwa na mstaafu mwenzetu Tommy Lee Jones kule Hollywood iitwayo. No Country For Old Men. 

Hadithi yake haihusiani sana na mambo ya wastaafu,  lakini kila mara mstaafu hujikuta akikumbuka jina la filamu hiyo linalomfanya aamini kuwa, sasa nchi yake aliyoijenga mwenyewe haina haja wala muda na wazee au wazee hawana tena pa kwenda!

Mstaafu ameishia kuwa 'jiwe' la pembeni walilolikataa waashi, lakini kwa vile sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, 'vox populi vox dei (kimbugu kwa msisitizo) mstaafu anamuomba Mungu  kuwa kabla hajamfanya mkazi wa kudumu wa Kinondoni,  siku awezeshe 'waashi' tofauti kufanya mabadiliko na kumfanya mstaafu wetu awe 'jiwe walilokataa waashi limekuwa sasa jiwe kuu la pembeni! Midomo na mioyo huumba.


Wastaafu wana changamoto za kifedha

Juliana Moses. Hapa nazungumzia changamoto kubwa zinazowakumba wastaafu wengi nchini. Baadhi ya wastaafu hawana mafao ya kutosha, na hii inawalazimu kuishi kwa hali ngumu kihuduma na kifedha. Serikali inapaswa kuangalia upya mifumo ya pensheni na kuhakikisha kuwa mafao yanawafikia kwa wakati.  Pia, kunahitaji kuwepo na mikakati ya kusaidia wastaafu kupata ajira za muda au fursa za kujiajiri ili kuondoa umaskini. Wastaafu ni mali ya taifa, na tunapaswa kuwaheshimu kwa kuwasaidia kuishi maisha bora.


Afya na huduma kwa wastaafu
Musa Musa. Huduma za afya kwa wastaafu zinahitaji kuboreshwa kwa dharura. Wengi wetu tumeona wastaafu wakilalamika kuhusu ukosefu wa huduma za afya bora, hasa zile zinazohusiana na magonjwa ya wazee. Serikali na taasisi binafsi zinapaswa kushirikiana kuanzisha vituo maalumu vya afya kwa wastaafu ili kuhakikisha wanapata matibabu stahiki. Huduma bora ya afya ni haki ya kila mstaafu na ni njia ya kuwahimiza kuishi maisha yenye heshima na afya njema.
Tafadhali zingatia suala hili.
 

Kujumuika kijamii kwa wastaafu
Pili Seif. Wastaafu wengi wanakumbwa na upweke na kutengwa kijamii baada ya kuacha kazi. Hali hii huathiri afya zao za akili na mwili. Tunashauri kuwepo kwa vikundi vya kijamii na shughuli za kijamii zinazowahusisha wastaafu ili kuwajumuisha na kuondoa upweke. Vilevile, familia na jamii ziwe na jukumu la kuwahudumia wastaafu na kuhakikisha wanahisi kuwa sehemu ya jamii. Upendo na ushirikiano ni muhimu kwa ustawi wa wastaafu.
Tushirikiane kuboresha maisha yao.


Wastaafu wanapaswa kuishi mazingira bora

Ashura Ibrahimu. Ni muhimu kuweka mazingira bora kwa wastaafu, hasa makazi na usalama wao. Wengi wanakaa katika mazingira duni yasiyo rafiki kwa afya na usalama wao. Serikali inapaswa kuanzisha makazi ya wastaafu yenye huduma muhimu kama maji safi, usafi, na usalama wa hali ya juu. Hii itasaidia kupunguza matatizo ya kiafya na kuwapa wastaafu amani ya akili. Makazi bora ni haki ya kila mstaafu.
Tunatoa wito kwa mamlaka husika kuchukua hatua.


Fursa za kujifunza na kuendeleza ujuzi

Godfrey Patric. Ingawa wastaafu wameacha kazi rasmi, bado wanaweza kuendelea kuchangia jamii kwa kujifunza na kuendeleza ujuzi mpya. Programu za mafunzo na elimu kwa wastaafu zinaweza kuwasaidia kupata ujuzi wa kisasa na kujihusisha na shughuli za kijamii au za kiuchumi. Hii itawapa motisha na kuondoa hali ya kukosa shughuli. Serikali na taasisi za elimu ziweke mikakati ya kuwasaidia wastaafu kujifunza mambo mapya.
Tushirikiane kuleta mabadiliko chanya.


0754 340606 / 0784 340606