Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Utapiamlo; tatizo linaloikosesha haki sawa elimu Tanzania

Muktasari:

KUTOKANA na matokeo ya shule zetu ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa mabovu na hivyo kutikisa taifa, tuna wajibu sisi wazazi, walezi na viongozi kutafakari sababu za msingi zinazosababisha vijana wetu wasifanye vizuri shuleni.

KUTOKANA na matokeo ya shule zetu ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa mabovu na hivyo kutikisa taifa, tuna wajibu sisi wazazi, walezi na viongozi kutafakari sababu za msingi zinazosababisha vijana wetu wasifanye vizuri shuleni.

Kuna tafiti ambazo zimefanywa nchi mbalimbali, Tanzania ikiwamo, hatuna budi sasa kuchukua hatua madhubuti ili taifa liweze kulikabili.

Utafiti uliofanywa na Hellen Murray, (2012) wa shirika la Young Lives kuhusu upatikanaji wa elimu sawa huko Ethiopia, Peru, India na Vietnam unaonyesha masuala ya msingi yanayosababisha kutokufikiwa kwa haki ya elimu sawa kwa watoto wote.
Pamoja na kwamba ni mazingira tofauti, sababu hizi zinatugusa pia kama nchi na hatuna budi kutafakari sisi tumepiga hatua gani katika kutatua matatizo haya.
Tatizo mojawapo ni matunzo ya awali ya mtoto. Katika hili, kuna masuala mawili ya msingi katika hili, kwanza ni lishe bora kwa mtoto chini ya mwaka mmoja.
Utapiamlo, kwa mfano unaweza ukasababisha matatizo makubwa katika ukuaji wa akili na hasa katika uwezo wa akili kufanya kazi vizuri.
Kutokana na ripoti ya Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) mwaka 2012, taarifa ya umaskini na maendeleo ya binadamu, hali ya utapiamlo inatisha Tanzania.
Taarifa hii inasema kwamba kati ya watoto wanne Afrika, mmoja ana utapiamlo. Tanzania ni nchi mojawapo ambayo ipo nyuma kwa kiwango kikubwa katika suala hili.
Taarifa hii inaonyesha kwamba asilimia 42 ya watoto wa Tanzania chini ya umri wa miaka 18 wana utapiamlo. Ni watoto 130 wanafariki kila siku kwa sababu ya tatizo hili.
Hali hii siyo nzuri kabisa na inachangia kwa kiasi kikubwa matokeo duni ya elimu Tanzania.
Kutokana na taarifa ya kisera ya Twaweza (2010) inayohusu masuala ya utapiamlo, mwaka 2004/05 watoto takribani million 2.4 walikuwa ni wafupi wa kimo ukilinganisha na umri wao, sababu kubwa ni utapiamlo. Hii ni idadi kubwa ya watoto.
Upungufu katika hili unasababishwa na vitu vingi, pamoja na uzalishaji na usambazaji duni wa chakula, kutowekeza vya kutosha katika elimu kwa akina mama wajawazito na kutowafikishia huduma stahiki kwa wakati.
Kwa mfano, taarifa ya Twaweza inaonyesha idadi kubwa ya akina mama wajawazito walikuwa na mapungufu ya vitamin na madini muhimu ambayo huchangia katika ustawi na afya ya mtoto atakayezaliwa.


Mengine ni sera zisizokidhi haja na utekelezaji hafifu wa sera na mikakati, pia huduma duni za afya kwa watoto wachanga na watoto chini ya umri wa miaka mitano, kwa mfano ni wazazi wachache wanaofikia huduma ya vitamini zinazohitajika kwa mtoto ili wakue vizuri.
Watoto wengi wanazaliwa na uzito kidogo, wanakosa damu ya kutosha, hawapati virutubisho vya muhimu katika makuzi.
Ni vyema kuelewa kwamba suala hili ni la kitabaka kwa vile wengi wanaokumbwa na tatizo la utapiamlo ni watu kutoka familia zenye kipato duni.
Mambo mengine ni masuala ya kijinsia, mila na tamaduni ambapo nchi nyingi za Afrika zimewapa kipaumbele watoto wa kiume zaidi katika ufikiaji wa lishe bora.
Iwapo Wizara zote na taasisi muhimu zitashirikiana kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili, tunaweza kusuluhisha.
Hii inahitaji nia na utashi. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ina jukumu kubwa la kutujengea miundombinu na mazingira ya elimu bora, lakini wizara nyingine na taasisi zinazohusika na makuzi ya mtoto zina changamoto kubwa ya kujenga misingi imara ya mtoto kuweza kufikia elimu bora.