Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tusichoke kuwaongoza kimaadili watoto wetu

Huwa inatokea kitu unapokisikia mara kwa mara kinakera na kuchosha masikioni, hasa kitu hicho kikiwa kibaya, hapa nazungumzia suala la mapenzi ya jinsia moja ambalo kwa sasa limechukua sehemu kubwa ya mijadala inayoendelea.

Kila utakapokaa ni lazima mada inayohusu masuala haya itajitokeza, binafsi sipendi kusikia habari hizi na nina uhakika kila mzazi na yeyote mwenye kujali maadili hatapenda kusikia mjadala huu, ila bahati mbaya ni kwamba janga hili tunalo na kulikalia kimya haiwezi kuwa suluhu.

Si mara moja au mbili tumewasikia viongozi wa Serikali wakikemea vitendo hivi, viongozi wa dini nao wameingilia kati kukemea na kuwakumbusha waumini wao kuvichukia.

Naunga mkono jitihada zote ambazo zinaendelea kufanyika hadi sasa kutoka kwa viongozi hao, ambao kimsingi wanafanya kazi hiyo kwa ngazi ya juu kwa maana wanashughulika na jamii na taifa kwa jumla, lengo likiwa kulinda kizazi chetu kisitumbukie kwenye uovu, tukapoteza nguvukazi ya taifa.

Hata hivyo, nachelea kusema kwamba jitihada hizo zinaweza zisizae matunda kama kwenye ngazi ya familia hatutaonyesha kuchukia na kupambana na vitendo hivi, hili litawezekana kupitia malezi, tuwanusuru watoto wasiangukie upande huo.

Najua si jambo tunalopenda kulisikia, ila ukweli ni kwamba wazazi wengi tunashindwa kusimama kwenye wajibu wetu wa malezi, watoto wanajilea wenyewe au tunaacha jukumu hilo kwa watu wengine, matokeo yake watoto wanafanya kile wanachoona ni sahihi kwao au wanachoshawishiwa kufanya.

Haya yote yanafanyika mzazi ukiwa huna ujualo, ukija kushtuka tayari mtoto ameshaharibika na huna namna ya kumsaidia, utaishia kumchukia na kumlalamikia Mungu, lakini wakati unalalamika ni lazima ujiulize ulitimiza wajibu wako?

Nakumbuka kauli ya Sheikh Khamis Mataka, “Siku hizi wazazi wanafuga hawalei, matokeo yake watoto wanayachukua zaidi mambo ya hovyo wanayokutana nayo duniani na kuamini ndiyo sahihi”.

Nakubaliana kabisa na kauli hii ya Sheikh na inawezekana hiki tunachokiona sasa hadi kufikia viongozi wakubwa wa Serikali, viongozi wa dini na bunge kulaani hadharani vitendo vya mapenzi ya jinsia moja ni matokeo ya kuteleza kwetu kwenye malezi.

Najua wapo watakaosema kuna wengine wanazaliwa wakiwa na vichocheo hivyo, kwa hiyo hilo ni suala la kibailojia, sipingani na mawazo haya, lakini bado mzazi ukisimama kwenye nafasi yako utaligundua hili mapema na kutafuta namna bora ya kumnusuru mtoto asitumbukie kabisa upande huo.

Hata hivyo, hawa wanaotokana na sababu ya kibailojia ni wachache, wengi wanaingia huko huenda kwa kushawishiwa au kulazimishwa kupitia vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa tangu wakiwa watoto, bado tunarudi palepale, wazazi tumeshindwa kuwalinda watoto wetu.

Kuna msemo unasema usiangalie ulipoanguka, bali ulipojikwaa, kama hivyo ndivyo nadhani tuna kila sababu ya kukubali tulijikwaa kwenye malezi na tunawajibika kurudi kwenye mstari ili kuhakikisha watoto na vijana wetu wanakuwa salama na kujiweka mbali na mazingira yanayoweza kuwaingiza kwenye upuuzi huo.

Tujenge ukaribu na watoto na vijana wetu, hii itasaidia kubaini mabadiliko yoyote ambayo yanaweza kujitokeza, pia ukaribu na mtoto unaweza kumpa uhuru wa kukuelezea kama kuna changamoto anayopitia au ushawishi wa aina yoyote ile ambayo inaweza kumhusisha na vitendo vya mmomonyoko wa maadili.

Usimuangalie mtoto wako wa kiume anayeanza kutembea kama mtoto wa kike au kupendelea mavazi ya kike au kijana wa kiume kupenda kuwa karibu na wanawake.Muhimu zaidi ni kuhakikisha muda wote watoto wanakuwa salama, zile zama za mgeni kulala na mtoto zimepita kwa kifupi hakuna yeyote unayepaswa kumuamini linapokuja suala la usalama wa mtoto wako.