Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tuzibe mianya hii ya rushwa katika uchaguzi

Tayari kipyenga kuashiria uchaguzi wa serikali za mitaa, kimepulizwa na wizara inayosimamia kinyang’anyiro hicho hapa nchini.

Kwa mujibu wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Mohammed Mchengerwa, uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

"Kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa za mwaka 2019, ibara 4 (1-3) (Matangazo ya Serikali Na. 571, 572, 573 na 574) ya mwaka 2024, ninautangazia umma wa Watanzania na vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu kuwa tarehe 27 Novemba 2024 itakuwa ni siku ya uchaguzi wa serikali za mitaa Tanzania Bara," alisema Mchengerwa.

Huu utakuwa ni uchaguzi wa saba kufanyika hapa nchini tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vigi vya siasa mwaka 1992. Uchaguzi wa kwanza ulikuwa mwaka 1994 na uchaguzi wa mwisho ulifanyika Novemba, 2019.

Ukiisoma kwa makini Katiba, Ibara 145 na 146, utabaini wazi kwamba, uwepo wa serikali za mitaa, umelenga kupeleka madaraka kwa wananchi.

Hata hivyo, malengo haya hayatimii kwa sababu ya mifumo ya kupatikana kwa viongozi wenyewe imejaa kasoro, kibao ikiwemo vitendo vya rushwa na mfano wa hivyo.

Kuwepo kwa vitendo vya rushwa wakati wa kuchagua viongozi, huwanyima haki wagombea na kuwakosesha maendeleo wananchi.

‘Nyimbo na mapambio’ ya ‘uchaguzi utakuwa huru na wa haki”, zinazoimbwa na viongozi kila wanapopata nafasi kusimama majukwaani vimewachosha wananchi kwa kuwa haviakisi uhalisia wanapoingia kwenye uchaguzi!

Kwa upande mwingine, nikiri kwamba, zipo jitihada za Serikali kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na wa haki kwa wananchi kumchagua kiongozi wamtakaye kupitia sanduku la kura kwa kuweka sheria mbalimbali ikiwemo ile ya kuzuia na kupambana na rushwa.

Sheria nyingine zilizowekwa na Serikali kwa madhumuni hayo ni zile za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, 2024, Sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi ya Taifa, 2024, Sheria ya Gharama za Uchaguzi namba 6 ya mwaka 2010 na sheria ya Vyama vya Siasa sura ya 258.

Lakini pamoja na sheria zote hizi, vitendo vinavyoashiria uwepo wa rushwa kwenye chaguzi zetu vinazidi kutamalaki kila uchao na uchwao, jambo linalofanya wananchi kukosa aina ya viongozi wanaowataka.

Kwa mfano, uchambuzi wa mfumo na ufuatiliaji uliofanywa na Takukuru kama sehemu ya majukumu yake kwenye chaguzi za mwaka 2014 na 2019 pamoja na Uchaguzi Mkuu mwaka 2020, uligundua kuwepo kwa malalamiko ya vitendo vya rushwa

Akizungumza na wanahabari hivi karibuni, Mkuu wa dawati la elimu kwa umma wa Takukuru mkoani Morogoro Bigambo Thomas, alisema matumizi ya rushwa peke yake katika chaguzi hizo yalikuwa asilimia 72.6.

Kwa mujibu wa Bigambo vihatarishi vya rushwa vilionekana kwenye maeneo ya utangazaji wa majina na mipaka ya mitaa, vijiji na vitongoji, kujiandikisha na maandalizi ya orodha ya wapiga kura, uteuzi wa wagombea katika nafasi mbalimbali, kampeni za wagombea, upigaji kura na kutangaza matokeo.

Kama maelezo ya afisa huyu wa Takukuru hayawezi kutiliwa shaka, maana yake Watanzania tuna safari ndefu kuhakikisha tunasaidiana na taasisi hii katika kudhibiti mianya ya rushwa hasa vyama vya siasa.

Nasema vyama vya siasa kwa sababu uchunguzi uliofanywa na Takukuru unabainisha kuwa, kati ya mbinu zinazofanikisha vitendo vya rushwa, kugawa fedha tasilimu ilikuwa ni aslimia 64.4, kugawa vitu mbalimbali kama fulana, kofia na vitenge asilimia 20 na kugawa vyakula na vinywaji asilimia 13.3.

Aidha lazima udhibiti huo uanzie kwenye maeneo kama ya uteuzi wa wagombea ngazi ya chama: Kwenye mchakato wa ndani ya chama kutia nia, kuchukua fomu na ujazaji, mchujo, kura, kutangaza matokeo na kufanya uteuzi wa mgombea kwa tiketi ya chama, kuna figisu-figisu mno!

Maeneo mengine ni wakati wa kampeni: matumizi ya fedha kwenye kampeni za uchaguzi ngazi ya chama, ni mahala pa kutazamwa sana.

Mwaka 2020 ndani ya chama kimoja cha siasa mgombea ubunge alipoona hakubaliki aligawa Sh1 milioni kwa kila katibu kata wa chama chake ili kuwarubuni wajumbe.

Haya maeneo wenye mamlaka pamoja na wananchi kwa ujumla wake, wanapaswa kuyatupia macho sana ili kupitia hayo, kuzizalike matobo ya rushwa yatakayoharibu malengo mazima ya uchaguzi kwa Taifa.