Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Suruali za kubana kwa wanaume ni hatari

Muktasari:

Madaktari wamesema uvaaji wa suruali za kubana kwa wanaume ni chanzo cha baadhi kuwa wagumba na wengine kupata magonjwa ya ngozi

Kampala. Kwa wananchi wa Uganda, jina la Denzel Mwiyeretsi siyo geni kwa kuwa ni mtangazaji wa masuala ya mjini katika Kituo cha Televisheni cha XFM, lakini Denzel pia ni maarufu kwa wafuatiliaji wa Big Brother kutokana na kushiriki shindano hilo nchini Afrika Kusini.

Hata hivyo, watu wengi wanamfahamu kwa mitindo ya uvaaji wake wa suruali za kubana.

“Mitindo ni kama umri, haiwezi kuwa vilevile. Ni kama vile mvinyo mtamu, pamoja na umri, mtindo wako lazima uwe na mwonekano mzuri. Ni kujaribu kitu kipya. Mimi ni mtu mwenye kuthubutu na napenda kujaribu vitu vipya (ikiwamo mitindo) ili kufanya maisha yangu yawe yenye mvuto,” alisema Denzel.

Pamoja na tabia yake ya kupenda kuvaa suruali za kubana kuna watu akiwamo dada yake hakupendezwa na hali hiyo, siku moja dada yake alimwambia hapendezwi na uvaaji huo.

“Miaka miwili iliyopita, dada yangu aliniambia kuwa uvaaji wangu wa suruali za kubana unaweza kuwafanya watu wanihisi mimi ni ‘shoga’. Lakini nilimueleza uvaaji huo ni mtindo wa maisha yangu,” alisema Denzel aliponukuliwa na gazeti la New Vision la Uganda.

Ingawa dada yake anauona uvaaji wake unalingana na wanaume wenye vitendo vya ushoga, aliendelea kutetea kuwa mpenzi wake wa kike amekuwa akimsifia kwa uvaaji wake wa suruali za mtindo wa kubana.

Hata hivyo, siyo watu wa kawaida pekee ndiyo wenye kukwazwa na mtindo wa uvaaji wa nguo za kubana wa Denzel. Hata madaktari nao wametoa ushauri wao kuwa uvaaji wa suruali za kubana ni hatari kiafya.

Lakini hoja za madaktari hazionyeshi kumteteresha Denzel ambaye alijibu kwa kusema kuwa ni madaktari hao hao wanaosema kunywa maji kwa kutumia vyombo vya planstiki ni hatari. Je? tumeacha kunywa maji kwenye chupa za plastiki? Kila tunachofanya ni hatari. Kitu kizuri ni kwamba sijawahi kuugua kwa sababu ya uvaaji wa mtindo wangu wa suruali za kubana.”

Historia ya suruali za kubana

Mchambuzi wa masuala ya mitindo, Keturah Kamugasa alisema suruali za kubana ni mtindo wa zamani ambao umerudi kwa kasi, hasa kupitia suruali aina ya jinsi. “Zamani zilikuwa zikiitwa ‘bomba’.”

Suruali za kubana mwanzoni zilivaliwa na wanasiasa wa kundi la mlengo wa kushoto la Sans-culottes, ambao walikuwa wapinzani wakubwa wakati wa Mapinduzi ya Ufaransa, wakati huo suruali hizo waliziita ‘pantaloons’.

Uvaaji huo ulianza kama uasi na kuwa mtindo wenye umaarufu katika miaka ya 1950. Suruali hizo baadaye zikaanza kuvaliwa na mastaa wa rock’n’roll katika miaka ya 1960 na kuendelea kusambaa katika jamii.

Baadaye, mtindo huo ulishika kasi na suruali za kubana, mkunjo mwembamba wa koti kifuani na tai nyembamba ukawa mtindo wa mavazi ya jamii nyingi katika kipindi hicho.

Katika miaka ya 1970, vijana wa kiume walionekana kuvaa suruali za kubana kuanzia kiunoni na mapajani, lakini chini zinakuwa pana. Kuanzia hapo mtindo wa suruali za bugaluu au suruali pana, ukazaliwa. Katika miaka ya 1980 mtindo wa rangi za kumeremeta kwa wanaume ukaibuka.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mlimbwende wa Uganda, Miss Uganda, Brenda Nanyonjo alieleza kuwa katika miaka 2000, enzi za kuweka rangi za kumeremeta, mkunjo wa koti kifuani na suruali za kubana kwa wanaume uliibuliwa upya na wabunifu wa mintindo wa kimataifa.

Mtindo wa wanaume wa kuweka rangi za kumeremeta kwa wanaume ukashika kasi katika ubunifu wa mitindo ya kileo kwa wanaume.

Matatizo ya kiafya

Dk Vincent Kafuuza wa Kituo cha Friends Polyclinic & Ambulance Service alisema siyo tu kuhusu suruali za kubana, lakini nguo zozote za kubana siyo nzuri kuwa mavazi ya kila siku.

Alieleza kuwa mwili unahitaji kupumua, hali ambayo hufanyika kupitia kutoka jasho kwenye vinyweleo kwenye ngozi na jasho linatakiwa kukauka lenyewe taratibu.

Dk Kafuuza alisema ikiwa mtu amevaa jinzi ya kubana au nguo ya ndani ya kubana, jasho litagandana kwenye vinyweleo vya ngozi na wakati mwingine inaweza kusababisha magonjwa ya ngozi kama vile ‘fangasi’, maumivu ya mwili na vipele katika mapaja na sehemu zingine za siri.

“Wanaume ambao wanavaa suruali za kubana wana hatari ya kupunguza kiwango cha mbegu za uzazi.

Na wakati mwingine zinaweza kupungua kwa kiwango kikubwa na kumfanya mwanamume ashindwe kumpa ujauzito mwanamke,” alisema Dk Kafuuza.

Dk Kafuuza alisema suruali za kubana zina kawaida ya kusukuma ndani sehemu zinazotunza mbegu za uzazi za mwanamume, hali inayosababisha matatizo kama vile uvimbe na ngozi kubabuka.

Nguo za ndani za kubana zinazuia kukuwa kwa mbegu za uzazi.

Wakati joto la kawaida la mwili ni sentigredi 37, mfuko wa mbegu za uzazi wa mwanamume unahitaji kiwango cha joto kati ya sentigredi 35.5 na 36 ili kufanya kazi katika hali ya kawaida.

Dk Charles Kiggundu ambaye ni Mshauri wa Hospitali ya Mulago na Chuo Kikuu cha Afya cha Makerere, alisema joto la mbegu za uzazi za mwanamume linaweza kuongezeka ikiwa mfuko unaozishika utafifia ndani ya mwili kwa muda mrefu, kwa mfano kama mwanamume amevaa nguo ya ndani ya kubana.

Kwa mujibu wa Dk Lawrence Kazibwe wa Hospitali ya Mulago, alisema mbegu za uzazi za mwanamume ziko kwenye mfuko maalumu kwa sababu zinahitaji kuwa zimepoa zaidi ya maeneo mengine ya mwili, ili ziwe kwenye mazingira tulivu.

Alisema lengo hilo linaweza kuvurugika iwapo mwanamume atavaa suruali ya kubana ambayo itazifanya mbegu za uzazi zikose mawasiliano ya kawaida na sehemu nyingine ya mwili, ambayo ni kupata joto linalotakiwa.

“Baadhi ya wanaume wanafikiri kusafirisha mbegu za uzazi pekee kwa mwanamke ndiko kunawezesha mwanamke kupata ujauzito, lakini urutubishaji hauwezi kutokea katika sehemu za kikeni,

kwa kuwa mbegu za uzazi lazima zipite kwenye mrija unaotakiwa kukutana na mayai mengine.

Hivyo basi mbegu za uzazi zinahitaji kuwa na nguvu na nyingi ili ziweze kuyafikia mayai ya kikeni na kuwezesha kupata ujauzito,” alifafanua Kiggundu.

Kiggundu alisema; “Hebu fikiria katika hali ambayo mbegu za uzazi ni chache na dhaifu! Hii ina maana hazitaweza kurutubisha mayai ya kike.

Hivyo unaweza kutoa mbegu za uzazi wakati wa tendo la ndoa, lakini hakuna ubebaji mimba utakaofanyika.”

Mbegu za uzazi ambazo ni dhaifu, kama vile zile ambazo hazina mkia, zenye mkia mkubwa, zenye mkia mdogo, zilizopinda kichwani na zile zenye mikia miwili, haziwezi kupenye kwenye mrija wa kwenda kwenye mayai ya uzazi ya kike.

Imeandikwa na Noor Shija kwa msaada wa mtandao.