Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwakalebela ataka kuisuka upya Yanga

Dar es Salaam. Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Frederick Mwakalebela amesema endapo atachaguliwa kuingia madarakani, kazi yake ya kwanza ni kubadili mfumo wa uendeshaji.

Mwakalebela alisema atamshauri mwenyekiti wake kutengeneza mfumo mzuri wa Yanga kujiendesha kwa kutumia rasilimali zake.

Katibu Mkuu huyo wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), alitoa kauli hiyo alipokuwa akizindua kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu.

“Nikipata nafasi ya kuingia katika uongozi tutakuwa na utaratibu maalumu wa michango ili kujua tuna wanachama wapi kwa wingi, lakini pia jinsi ambavyo watachanga fedha ziende sehemu sahihi, alisema Mwakalebela.

Mwakalebela alisema ni muumini wa kutaka mabadiliko na wataomba ridhaa ya wanachama kupitia mkutano mkuu ambao utatoa baraka kwao kufanikisha malengo yao.

Pia alisema atampa majukumu mapya kocha mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ili kumpa mamlaka ya kufanya kazi kwa weledi.

Kigogo huyo alisema Zahera amekuwa chachu ya mafanikio ya Yanga katika Ligi Kuu Tanzania Bara na amekuwa akimvutia katika usimamizi wake wa nidhamu ndani ya klabu hiyo kongwe nchini.

Mbali na Katibu Mkuu wa TFF, Mwakalebela alikuwa kiongozi mwandamizi wa klabu ya Mtibwa Sugar, Mwenyekiti Chama cha Soka Wilaya Mvomero,Meneja timu ya Mkoa Morogoro na Mjumbe Kamati ya Kusaidia klabu ya Lipuli.