Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

 Yanga yaibua mambo matano, Bodi ya Ligi yajibu

Muktasari:

  • Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu baina ya Yanga na Simba kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar ulimalizika kwa sare ya bila kufungana, Machi Mosi, 2026.

Dar es Salaam. Yanga leo Jumamosi, Machi 07, 2026 imesema imeandika barua kwa Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ikihitaji ufafanuzi wa mambo matano.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa wamelazimika kufanya hivyo kwa vile wanachama wao wanahitaji ufafanuzi wa mambo hayo.

Jambo la kwanza ni adhabu ya mshambuliaji wa Simba, Selemani Mwalimu ya kufungiwa mechi tatu kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Dodoma Jiji ambapo Yanga imetaka ufafanuzi wa kwa nini kamati imetumia kanuni tofauti ya 41:5(5.2) iliyomfungia mechi tatu badala ya kutumika kanuni ya 41:21 ambayo ingefanya afungiwe mechi tano.

Ufafanuzi wa pili ambao Yanga wameutaka ni juu ya kuchelewa kwa kamati hiyo kutoa uamuzi wa suala la Selemani Mwalimu huku jambo la tatu ni ufafanuzi wa adhabu tofauti ambazo marefa wasaidizi wawili wa mechi baina yao na Simba, kwa kosa moja la kushindwa kutafsiri sheria ya kuotea.

Jambo la nne ambalo Yanga wamehitaji ufafanuzi wake ni la taarifa ya TPLB kudai refa msaidizi alikataa bao halali la Simba kinyume na muongozo wa sheria na taratibu za soka duniani.

"Kwa mujibu wa sheria za FIFA, goli halali ni lile goli pekee ambalo limeruhusiwa na mwamuzi wa kati. Kinyume na hapo hakuna kamati wala sheria au kanuni ambayo inayo mamlaka ya kuhalalisha goli ambalo halikuidhinishwa na mwamuzi wa kati.

"Kauli ya kwamba Simba wamenyimwa goli halali imeleta taharuki kwa umma. Tumeiandikia kamati itueleze imetoa wapi mamlaka ya kutangazia Uumma kuwa goli ni halali," amesema Kamwe.

Jambo la tano ni ufafanuzi wa kutoadhibiwa kwa refa msaidizi aliyeruhusu bao la pili la Simba dhidi ya KMC, Yanga ikidai kuwa bao hilo lililofungwa na Selemani Mwalimu lilikuwa la kuotea.

Ofisa Habari wa TPLB, Karim Boimanda amesema kuwa itafuata taratibu za kikanuni katika kushughulikia suala hilo.

"Kikanuni klabu inaweza kuomba mrejesho kwa kamati hivyo Bodi kwa sasa haiwezi kuzijibu kwa vile zimeelekezwa kwa kamati ambayo bado haijakutana," amesema Boimanda.