Ajibu atua apewa jezi ya Sure Boy Azam

Thursday December 30 2021
ajibu pic
By Daudi Elibahati

KIUNGO Mshambuliaji wa Tanzania, Ibrahim Ajibu 'Cadabra' amejiunga na klabu ya Azam FC kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Simba.

Taarifa iliyotolewa na Simba imeeleza kufikia makubalino na nyota huyo ya kuvunja mkataba wake kuanzia leo Alhamisi Desemba 30, 2021.

Ajibu alijiunga na Simba Julai 3, 2019 akitokea kwa watani zao wa jadi Yanga baada ya mkataba wake wa miaka miwili kumalizika wa kuichezea timu hiyo.

Nyota huyo amekabidhiwa jezi namba 8 iliyokuwa inavaliwa na kiungo Salum Abubakar 'Sure Boy' ambaye amejiunga na vinara wa Ligi Kuu Bara klabu ya Yanga kwa mkataba wa miaka miwili.

Advertisement