Aliyeshtakiwa na Yanga aula Fifa

Muktasari:

  • Michezo ya Olimpiki imepangwa kufanyika Ufaransa kuanzia Julai 26 hadi Agosti 11 ikishirikisha wanamichezo wapatao 10,500 watakaoshiriki katika michezo 32 tofauti.

Refa Dahane Beida wa Mauritania ni miongoni mwa waamuzi 12 kutoka Afrka waliteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (Fifa) kuchezesha mechi za michezo ya Olimpiki kuanzia Julai 26 hadi Agosti 11 mwaka huu huko Ufaransa.

Dahane mwenye umri wa miaka 32 hivi karibuni alituhumiwa na Yanga kupanga matokeo ya mechi yao ya marudiano ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns Ijumaa iliyopita,

Yanga ilienda mbali zaidi na kulitaka shirikisho la mpira wa miguu Afrika (Caf) kumchunguza na kumchukulia hatua Dahane baada ya mwamuzi huyo kukataa bao la kiungo wake Aziz Ki Stephane kwenye mechi hiyo iliyomalizika kwa sare tasa katika dakika 90 za mchezo huku Yanga ikipoteza kwa mikwaju ya penalti 3-2.

Hata hivyo wakati majibu ya rufaa ya Yanga yakiwa hayajatolewa, Fifa imemteua Dahane kuchezesha mashindano ya Olimpiki akiwa na marefa wengine 11 kutoka Afrika.

Mbali na Dahane, Waafrika wengine walioteuliwa kuchezesha michezo ya Olimpiki mwaka huu ni Karboubi Bouchraw wa Morocco, Mahmood Ismail(Sudan), Diana Chkotesha(Zambia), Fatiha Jermoumi(Morocco), Elvis Noupue (Cameroon), Stephen Yiembe.(Kenya), Mahmoud Ashour (Misri), Lahlou Benbraham (Algeria), Ahmed Abdoulrazack (Djibouti), Emiliano Dos Santos (Angola)  na Shamirah Nabadda Uganda).

Marefa 89 walioteuliwa kuchezesha mashindano hayo wamegawanywa katika makundi manne ambayo ni marefa wa kati, marefa wasaidizi, marefa wa teknolojia ya usaidizi wa video kwa waamuzi pamoja na marefa wa kutoa sapoti.

Katika orodha hiyo, marefa wa kati ni Abatti Ramon, Alves Edina, Al Naqbi Adel, Beida Dahane,  Emikar Calderas, Espen Eskas, Yael Falcon, Mahmood Ismail, Drew Fischer, Katia Garcia, Karboubi Bouchra, Campell-Kirk, Yujeong Kim, Francois Letexier, Said Martinez, Glenn Nyberg, Tess Olofsonn, Tori Penso, Ilgiz Tantashev  Rebecca Welch na Yoshimi Yamashita.

Upanden wa wasaidizi kuna, Ahmed Abdoulrazack, Al-Ali Sabet, Ahmed Alrashadi, Rafael Alves, Lyes, Neuza Back, Michael Barwegen, Isaak Bashevkin, Mahbod Beigi, Fabrini Costa, Mary Blanco, Makoto Bozono, Guillerme Camilo, Emily Carney, Joanna Charaktis, Diana Chkotesha, Del Yesso Maximiliano, Francesca Di Monte, Karen Diaz, Jan Erik Engan, Timur Gaynullin, Fatiha Jermoumi, Walter Lopez na Mayo Brooke.

Wengine wasaidizi ni Cyril Mugnier, Kathryn Nesbitt, Bernard Mutukera,  Elvis Noupue , Franca Overtoom, Misuk Park, Mehdi Rahmouni, Christian Ramirez, Sandra Ramirez, Facundo Rodriguez, Migdalia Rodriguez, Emiliano Dos Santos, Andreas Soderkvist, Almira Spahic, Naomi Teshirogi, Isaac Trevis, Andrey Tsapenko na Stephen Yembe wa Kenya

Waamuzi wa VAR ni Khamis Al Marri, Mahmood Ashour, Ivan Bebek, Lahlou Benbraham, Jerome Brisard, Rodrigo Carvajal, David Coote, Carlos Grande, Rob Dieperink, Leodan Gonzalez, Tatiana Guzman,  Hategan Ovidiu, Kate Jacewicz, Katalin Kulcsar, Daiane Muniz, Guillermo Pacheco, Hector Paletta, Daneon Parchment, Sivakorn Pu-Udom na Paolo Valelo.

Marefa kwa ajili ya kutoa sapoti ni Veronika Bernatskaia, Jelena Cvetkovic, Anahi Fernandez, Odette Hamilton, Frida Klarlund na Shamirah Nabadda.