Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Alonso kimeeleweka Chelsea akiwaahidi mashabiki furaha

Muktasari:

  • Kwa sasa Chelsea inashika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu England (EPL) ikiwa imekusanya pointi 49.

Tetesi za Chelsea kumuajiri Xabi Alonso kama Meneja Mkuu mpya wa kikosi chao zimekuwa rasmi baada ya klabu hiyo kumtambulisha nyota huyo leo Jumapili, Mei 17, 2026.

Alonso ambaye msimu uliopita aliinoa Real Madrid kabla ya kutimuliwa, ataanza kuinoa Chelsea kuanzia Julai Mosi mwaka huu kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo.

Kocha huyo anaingia klabuni hapo kama mrithi wa kudumu wa nafasi ya Liam Rosenior ambaye alitimuliwa mwezi uliopita kutokana na mwenendo usioridhisha wa timu hiyo.

Meneja mpya wa Chelsea, Xabi Alonso wakati alipokuwa na Real Madrid. Picha na Mtandao

Kutangazwa kwa Alonso kumekuja saa chache baada ya Chelsea kupoteza mechi ya fainali ya Kombe la FA iliyochezwa jana Jumamosi katika Uwanja wa Wembley dhidi ya Man City kwa bao 1-0.

Muda mfupi baada ya kutambulishwa, Alonso amesema kuwa ni fahari kubwa kwake kujiunga na Chelsea akiamini atakuwa chachu ya kuipa mafanikio.

“Chelsea ni moja ya klabu kubwa zaidi katika soka duniani na inanipa fahari kubwa kuwa meneja wa klabu hii kubwa.

“Katika mazungumzo yangu na kundi la wamiliki pamoja na uongozi, ni wazi kwamba tunashiriki malengo yanayofanana. Tunataka kujenga timu yenye uwezo wa kushindana kwa kiwango cha juu kila wakati na kupigania mataji.

“Kuna vipaji vikubwa ndani ya kikosi hiki na uwezo mkubwa sana katika klabu hii ya soka, na itakuwa heshima kubwa kwangu kuiongoza. Kwa sasa, lengo ni kufanya kazi kwa bidii, kujenga utamaduni sahihi na kushinda mataji,” amesema Alonso.

Meneja mpya wa Chelsea, Xabi Alonso wakati alipokuwa akiichezea Liverpool. Picha na Mtandao

Xabi Alonso alicheza kwa miaka mitano katika Ligi Kuu England akiwa na Liverpool ambapo aliisaidia kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2005.

Pia aliwahi kuchezea Real Sociedad, Real Madrid na Bayern Munich.

Aidha, aliichezea timu ya taifa ya Hispania mara 114, akishinda Kombe la Dunia mwaka 2010 huku pia akitwaa mataji mawili ya Kombe la Euro.