Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool inavyopitia njia ya Ubingwa Ulaya

Muktasari:

  • Katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, Liverpool imefanikiwa kuzifunga Real Madrid, Atletico Madrid, Inter Milan, Marseille, Eintracht Frankfurt na Qarabag katika hatua ya ligi.

Istanbul, Uturuki. Klabu ya Liverpool imekuwa na msimu mgumu katika Ligi Kuu England lakini katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imeonyesha sura tofauti kabisa jambo linalowapa mashabiki sababu ya kuamini kuwa wanaweza kutwaa taji hilo.

Kwa mashabiki wa Liverpool, safari ya kwenda Istanbul huwa inawakumbusha moja ya usiku wa kihistoria katika soka la Ulaya.

Katika jiji hilo, kwenye Uwanja wa Atatürk Olympic, ndipo ambapo Liverpool waliandika historia mwaka 2005 ya kupindua matokeo baada ya kutoka nyuma kwa mabao 3-0 na kuifunga AC Milan katika fainali ya Kombe hilo.

Majogoo hao wa Anfield wakati huo walikuwa chini ya kocha Rafael Benítez, wakiwa na nyota kama Steven Gerrard, Jamie Carragher na Xabi Alonso.

Cha kushangaza ni kwamba msimu huo Liverpool walimaliza nafasi ya tano katika Ligi Kuu England, lakini mwisho wa msimu walitawazwa kuwa wafalme wa Ulaya.

Nyota wa Liverpool, Florian Wirtz, akiwashukuru mashabiki wa timu hiyo baada ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kumalizika kwa kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Galatasaray katika hatua ya ligi msimu huu. Picha na Mtandao


Sura tofauti Ulaya

Baada ya miaka kadhaa kupita, Liverpool sasa wanaonekana kurudia hali hiyo. Ingawa matokeo yao ya ligi yamekuwa yakisuasua, lakini katika Ligi ya Mabingwa wamekuwa wakionyesha kiwango bora.

Wamefanikiwa kuishinda Real Madrid, Mabingwa wa kihistoria wa mashindano hayo, pamoja na kuifunga Atlético Madrid kwa urahisi.

Pia waliibuka na ushindi dhidi ya Inter Milan na Olympique de Marseille ugenini, huku wakiiadhibu Eintracht Frankfurt kwa mabao 5-1.

Kiungo mshambuliaji wa Liverpool, Alexis Mac Allister, akizungumza kabla ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayozikutanisha Liverpool dhidi ya Galatasaray. Picha na Mtandao


Ndoto ya kutwaa taji

Kiungo wa Liverpool Alexis Mac Allister amesema kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya ni moja ya malengo makubwa ya timu hiyo msimu huu.

“Ni ndoto yangu kwa sasa. Ni mwaka wa Kombe la Dunia, kwa nini tusishinde tena? Ligi ya Mabingwa ni moja ya malengo makubwa ya msimu huu,” amesema Mac Allister.

Kocha wa Liverpool, Arne Slot, wakati akisikiliza swali katika mkutano na wanahabari kuelekea mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayowakutanisha na Galatasaray. Picha na Mtandao


Changamoto ya Galatasaray

Hata hivyo, Liverpool wanakabiliwa na mtihani mgumu wanapokutana na Galatasaray katika Uwanja wa RAMS Park, ambao unajulikana kwa presha kubwa kutoka kwa mashabiki.

Kocha wa Liverpool Arne Slot amesema mazingira ya uwanja huo ni magumu kwa timu ngeni.

“Mashabiki wao ni wa kutisha sana. Ukishika mpira wanapiga miluzi kwa sauti kubwa sana. Ni mazingira magumu kwa wachezaji,” amesema Slot.

Kipa wa Liverpool, Alisson Becker, ataikosa mechi ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Galatasaray baada ya kupata maumivu akiwa mazoezini. Picha na Mtandao


Liverpool wakosa baadhi ya nyota

Katika mchezo huo Liverpool hawatakuwa na kipa wao namba moja Alisson Becker, aliyepata maumivu wakati wa mazoezi. Pia mshambuliaji Federico Chiesa hatakuwepo baada ya kuugua.

Hata hivyo, pamoja na changamoto hizo, Liverpool wana sababu ya kuamini kuwa wanaweza kufika mbali au hata kutwaa tena taji la Ligi ya Mabingwa.

Mechi nyingine za hatua ya 16 bora zitapigwa kwenye viwanja tofauti ambapo pale England kwenye Uwanja wa St. Jame’s Park, Klabu ya Newcastle itavaana na Mabingwa wa La Liga, Barcelona.

Mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich watakuwa ugenini kukabiliana na Atalanta ambayo ilipenya katika hatua hii kwa kupindua meza dhidi ya Borussia Dortmund katika hatua ya mtoano.

Mchezo mwingine utapigwa Madrid, Hispania ambapo vijana wa Diego Simeon, Atletico Madrid watakuwa kwenye Uwanja wao wa Riyadh Air Metropolitano kuvaana na Tottenham