Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man City kuvaana na Liverpool, Arsenal, Chelsea zapewa hawa robo fainali FA

Mshambuliaji wa Manchester City, Herling Haaland, wakati akishangilia bao katika mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Liverpool iliyopigwa msimu huu katika Uwanja wa Anfield. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Mechi zote za robo fainali zinatarajiwa kuchezwa mwishoni mwa wiki ya Aprili 4 hadi 5.

London, England. Droo ya hatua ya robo fainali ya Kombe la FA imefanyika jana usiku, huku vigogo wa soka England wakipata wapinzani wao katika hatua hiyo ambayo itazikutanisha uso kwa uso Manchester City na Liverpool.

Mshambuliaji wa Port Vale, Ben Waine, akishangilia baada ya kuifunga Sunderland katika raundi ya tano ya Kombe la FA na kuipeleka timu hiyo katika hatua ya robo fainali ambapo itavaana na Chelsea, Stanford Bridge. Picha na Mtandao


Chelsea vs Port Vale

Klabu ya Port Vale imepangiwa kusafiri kwenda London kucheza dhidi ya Chelsea. Klabu hiyo ambayo kwa sasa inashika mkia kwenye msimamo wa League One, iliandika historia ya kufika robo fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1954 baada ya kuitupa nje Sunderland katika hatua ya raundi ya tano.

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola (kushoto) mwingine ni kocha wa Liverpool, Arne Slot, ambao watakutana mwezi ujao katika robo fainali ya mashindano ya Kombe la FA. Picha na Mtandao


Vita kali Etihad

Mchezo unaosubiriwa kwa hamu zaidi ni ule utakaopigwa katika Uwanja wa Etihad ambapo Manchester City watamenyana na Liverpool.

Man City wanawania taji lao la nane la FA chini ya kocha Pep Guardiola, huku Liverpool wakitafuta taji baada ya kupoteza nafasi ya ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

Baadhi ya wachezaji wa Arsenal, wakishangilia moja ya bao katika ushindi wa 2-1 katika raundi ya tano ya Kombe la FA walioupata dhidi ya Mansfield Town. Picha na Mtandao


Southampton vs Arsenal

Mabingwa wa kihistoria wa mashindano hayo Klabu ya Arsenal, imepangiwa kucheza ugenini dhidi ya Southampton, ambao ilifanya maajabu kwa kuiondoa Fulham katika raundi iliyopita.

Kikosi cha Mikel Arteta bado kinawania mataji katika mashindano yote manne wanayoshiriki msimu huu, na ushindi unaweza kuwapeleka Wembley kwa mara ya pili baada ya kufuzu kucheza mechi ya fainali ya Kombe la Carabao dhidi ya Manchester City itakayopigwa Machi 22, 2026.

Baadhi ya wachezaji wa West Ham, wakishangilia baada ya kufuzu hatua ya robo fainali kwa kuitupa nje Brentford kwa penalti 5-3. Picha na Mtandao


West Ham vs Leeds

Katika droo nyingine, West Ham itakuwa kwenye Uwanja wake wa nyumbani kuvaana na Leeds United. West Ham imefuzu kucheza robo fainali baada ya kuitupa nje Brentford jana usiku kwa mikwaju ya penalti 5-3 baada ya kutoka sare ya 2-2.

Kwa mujibu wa waandaaji wa mashindano, kila timu itakayofuzu nusu fainali itapata zawadi ya paundi 477,000 (Sh1.7 bilioni) huku ile itakayopoteza katika hatua inayofuata kwenye Uwanja wa Wembley itapewa paundi 530,000 (Sh1.9 bilioni).

Mechi zote za robo fainali zinatarajiwa kuchezwa mwishoni mwa wiki ya Aprili 4 hadi 5.