Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aziz Ki akutwa na Covid Morocco

Muktasari:

  • NYOTA wa Yanga na timu ya taifa ya Burkina Faso, Stephane Aziz Ki anatarajia kuripoti kambini Jumatatu ya wiki hii kutokana na changamoto za Covid-19 aliyoipata akiwa katika majukumu yake na timu ya taifa.

NYOTA wa Yanga na timu ya taifa ya Burkina Faso, Stephane Aziz Ki anatarajia kuripoti kambini Jumatatu ya wiki hii kutokana na changamoto za Covid-19 aliyoipata akiwa katika majukumu yake na timu ya taifa.

Aziz Ki alikuwepo kwenye kikosi hicho kilichocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Comoros uliopigwa Septemba 27, mwaka huu katika Uwanja wa Pere Jego jijini Casablanca nchini Morocco.

kwa taratibu za afya za Morocco wageni hupimwa Covid-19 kila baada ya siku tatu na Aziz Ki ni miongoni mwa wachezaji watatu wa Burkina Faso waliokutwa na maambukizi ya Corona baada ya kipimo hicho kufanyika baada ya mchezo.