Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baada ya Aziz Ki sasa Wydad wanamtaka huyu Yanga


IlichofanyaWydad msimu uliopita kwa Yanga ikimsajili kiungo mshambuliaji, Stephane Aziz KI, inataka irudie tena na safari hii imepiga hodi klabuni hapo kuulizia uwezekano wa kumchukua Maxi Nzengeli.

Taarifa zinabainisha, Waarabu hao wamefanya mawasiliano na wasimamizi wa Maxi wakionyesha nia ya kumtaka kiungo huyo kwa ajili ya msimu ujao.

Mtoa taarifa huyo alisema Maxi bado ana mkataba na Yanga wa mwaka mmoja, hivyo wasimamizi wake wameitaka klabu hiyo kuwasiliana na uongozi wa Yanga ili wafanye mazungumzo ya kukamilisha dili hilo kama watakubaliana.

“Maxi anatakiwa Morocco, wale Wydad walikuja na kuuliza juu ya mkataba wake, tukawaambia bado ana mkataba na klabu yake ya Yanga, unajua msimu uliopita aliongeza mkataba hapo,” alisema mmoja wa wasimamizi wa kiungo huyo.

“Tuliwapa namba ya mtendaji mkuu wa Yanga (Andre Mtine) wawasiliane nao, sisi hatuna shida kama Yanga itakubali kufanya biashara.”

Hivi karibuni, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe alisema suala la mustakabali wa wachezaji katika kikosi hicho, itafahamika mwisho wa msimu na benchi la ufundi litawasilisha ripoti itakayoonesha nani anastahili kubaki na nani aondolewe kutokana na mahitaji yalivyo.

Pia ishu ya kuuza au kutouza mchezaji, itaangaliwa ofa kama imekidhi na uwezekano wa kumpata mbadala wake.

Huu ni msimu wa tatu kwa Maxi kuitumikia Yanga akisalia na mkataba wa mwaka mmoja, lakini tangu atue ndani ya kikosi hicho amekuwa akipata nafasi wakati wote licha ya makocha kubadilika.

Mkongomani huyo mwenye uwezo wa kucheza eneo la kiungo mshambuliaji akitokea pembeni sambamba na beki, msimu huu katika mechi 25 ambazo Yanga imecheza za Ligi Kuu Bara, hajakosa hata moja, huku zote akianza kikosi cha kwanza.

Nyota huyo aliyetua Yanga Julai 2023 akitokea AS Maniema ya kwao DR Congo, katika msimu wa kwanza 2023-2024 alifunga mabao 11 kwenye ligi, kisha uliofuata 2024-2025 akapachika sita na asisti kumi, huku 2025-2026 ameshariki kwenye mabao kumi, akifunga matano sawa na asisti. Ikumbukwe, Waarabu hao kutoka Morocco walimchukua Aziz KI wiki kadhaa kabla ya msimu uliopita 2024-2025 haujamalizika na kumpa mkataba wa miaka miwili huku akijumuishwa kwenye kikosi kilichoshiriki Kombe la Dunia la Klabu nchini Marekani.

Wydad ilivutiwa na Aziz kutokana na rekodi zake za msimu wa 2023-2024, alipomaliza akiwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara akiwa na mabao 21, lakini alipoenda huko hakuonyesha makali yake, akauzwa kwenda Al-Ittihad ya Libya alipo sasa.

Akiwa Wydad, Aziz KI aliitumikia kwa kipindi cha takribani miezi saba akifanikiwa kucheza mechi saba za ligi na kufunga bao moja.