Baada ya NBA, King LeBron sasa atamba na sinema

Baada ya NBA, King LeBron sasa atamba na sinema

Muktasari:

Sinema iliyoachiwa na kampuni ya New Warner Bros ya "Space Jam: A New Legacy" imekwea hadi kileleni mwa filamu zilizotamba mwishoni mwa wiki, ikiingiza dola 31.7 milioni (sawa na Sh73.4 bilioni za Kitanzania), ikiwa ni kiwango kizuri katika sekta ya filamu tangu kuibuka kwa ugonjwa wa virusi vya corona, Covid-19.

Los Angeles, Marekani. Sinema iliyoachiwa na kampuni ya New Warner Bros ya "Space Jam: A New Legacy" imekwea hadi kileleni mwa filamu zilizotamba mwishoni mwa wiki, ikiingiza dola 31.7 milioni (sawa na Sh73.4 bilioni za Kitanzania), ikiwa ni kiwango kizuri katika sekta ya filamu tangu kuibuka kwa ugonjwa wa virusi vya corona, Covid-19.


 in the best showing of a family film since Covid first hammered Filamu hiyo ya matukio mubashara yaliyonogeshwa kwa vikaragosi na ambayo ni mwendelezo wa filamu ya "Space Jam" iliyotoka miaka 25 iliyopita ikimuhusisha gwiji wa NBA, Michael Jordan, inamuonyesha LeBron James akiungana na Bugs Bunny na vikaragosi vya vitimbi vya Looney Tunes katika filamu inayoangalia mchezo wa mpira wa kikapu dhidi ya wahusika hao wa akili bandia wanaotishia maisha ya mtoto wake was kiume.


Filamu hiyo iliipiku sinema ya "Black Widow" iliyokuwa inayoongoza wiki iliyopita kutoka kampuni ya Disney.


Filamu hiyo iliyotengenezwa na Marvel Studios, ambayo Scarlett Johansson ameingiza kama muhusika mkuu, ilikusanya dola 25 milioni, ikiwa ni anguko kubwa kutoka dola 80.4 milioni katika wiki ya kwanza, kwa mujibu wa mwangalizi wa sekta hiyo, Exhibitor Relations.


Katika nafasi ya tatu, filamu ya kusisimua ya kisaikolojia ya Escpae Room" kutoka Sony, iliingiza dola 8.8 milioni.


Nafasi ya nne ilikwenda kwa filamu ya Universal ya "F9: The Fast Saga," iliyokusanya dola 7.7 milioni na kufanya jumla ya mapato ya wiki nne ndani ya Marekani ya filamu hiyo ya matukio ya kusisimua ya Vin Diesel/John Cena kufika karibu dola 155 milioni.


Nyingine katika kumi bora ya filamu za mwisho wa wiki:
"The Forever Purge" (dola 4.1 milioni)
"A Quiet Place: Part II" (2.2 milioni)
"Roadrunner" (2 milioni)
"Cruella" (1.2 milioni)
"Pig" (970,000)

keywords: Entertainment|US|Canada|film|boxoffice