Badru mchezaji bora wa Februari Ligi Kuu Zanzibar

Mchezaji Ali Badru Ali wa timu ya Jang’ombe

Muktasari:

  • Badru alisajiliwa na taifa hivi karibuni katika usajili wa dirisha dogo baada ya kupata kibali cha uhamisho cha kimataifa (ITC) kutoka Oman alipokua akikipigia kwa muda mrefu.
  • Kabla ya kujiunga na klabu hiyo, Badru alikuwa akikipigia nchini Oman katika klabu ya Al Bashaer baada ya kuhama timu ya Asuwez Kamal nchini humo akitokea Jamhuri ya Pemba.

Zanzibar. Kamati ya Ufundi ya ZFA Taifa imemteua mchezaji Ali Badru Ali wa timu ya Jang’ombe kuwa mchezaji bora wa Februari 2017.

Badru alisajiliwa na taifa hivi karibuni katika usajili wa dirisha dogo baada ya kupata kibali cha uhamisho cha kimataifa (ITC) kutoka Oman alipokua akikipigia kwa muda mrefu.

Kabla ya kujiunga na klabu hiyo, Badru alikuwa akikipigia nchini Oman katika klabu ya Al Bashaer baada ya kuhama timu ya Asuwez Kamal nchini humo akitokea Jamhuri ya Pemba.

Uzoefu alioupata nchini Oman umeonekana kuwa ni miongoni mwa sababu zilizomfanya mchezaji huyo kung’ara katika soka ya Zanzibar msimu huu.

Kamati inayoongozwa na kocha Abdulghan Msoma ilimteua Saleh Mohamed Machupa wa Malindi kuwa kocha bora wa mwezi pamoja mwamuzi bra kuwa Haule Mbaraka Haule.

Kwa mujibu wa taarifa za kamati hiyo, zawadi kwa washindi hao zinatarajiwa kutolewa wakati wowote kuazia sasa.