Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bao la jioni lairudisha Liverpool kileleni EPL

Muktasari:

  • Liverpool inaongoza msimamo wa Ligi Kuu England ikiwa na pointi 12 ilizopata katika mechi nne.

Bao la mkwaju wa penalti uliopigwa na Mohamed Salah katika dakika za majeruhi leo Jumapili, Septemba 14, 2025, limeipa Liverpool pointi tatu muhimu ugenini dhidi ya Burnley ulioifanya irudi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England (EPL).

Penalti hiyo iliamriwa na refa Michael Oliver baada ya Hannibal Mejbri wa Burnley kuunawa mpira katika eneo la hatari alipokuwa katika harakati za kuokoa krosi ya Andrew Robertson. 

Ushindi huo umeifanya Liverpool kufikisha pointi 12 ambazo zimeirudisha kileleni mwa msimamo wa EPL ikiipiku Arsenal ambayo ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi tisa.

Katika mchezo huo,Burnley ilipata pigo katika dakika ya 84 baada ya Lesley Ugochukwu kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi ya njano ya pili.

Ushindi huo umeifanya Liverpool kuweka rekodi ya kuwa timu pekee kushinda mechi nne mfululizo za EPL kwa kutegemea mabao ya dakika 10 za mwisho au zaidi.

Hii ni mara ya tatu kwa Liverpool kupata ushindi katika mechi nne mfululizo za kwanza EPL ambapo mara mbili za mwanzo ilikuwa ni katika msimu wa 2018/2019 na msimu wa 2019/2020.

Matokeo hayo yameifanya Burnley kupoteza kwa mara ya kwanza mechi ya ligi baada ya kucheza mechi 24 mfululizo bila kuangusha pointi tatu ambapo ilikuwa imeshinda mechi 15 na kutoka sare tisa.

Bao la Mohamed Salah limeifanya Liverpool kuendelea kuboresha rekodi yake ya kuwa timu iliyofunga idadi kubwa ya mabao kuanzia katika dakika ya 90 ambapo leo imefikisha mabao 47.

Kichapo cha leo kimeifanya Burnley kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kupoteza mechi mbili mfululizo za ligi ambazo imeruhusu penalti kwa wapinzani baada ya dakika 90.

Salah sasa amefikisha idadi ya mabao 188 ya Ligi Kuu England ambayo yanamfanya asogee hadi nafasi ya nne katika chati ya wafungaji bora wa muda wote wa Ligi hiyo.