Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barker na mtihani wa kwanza Ligi Kuu

Muktasari:

  • Ni mechi inayokutanisha timu mbili ambazo hazijaachana kwa tofauti kubwa ya pointi ingawa Mtibwa Sugar imecheza idadi kubwa ya mechi ambazo ni nane hadi sasa huku Simba ikicheza mechi tano tu.

Dar es Salaam. Baada ya kushindwa kutamba Katika Kombe la Mapinduzi 2026, Kocha Mkuu wa Simba, Steve Barker leo atakuwa na kibarua cha kuiongoza kwa mara ya kwanza timu hiyo kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara wakati itakapovaana na Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam kuanzia saa 10:00 jioni.

Mchezo huo ni fursa muhimu kwa Barker na kikosi chake kurudisha nyuso za tabasamu kwa mashabiki wa Simba ambao walishuhudia timu yao ikichapwa kwa bao 1-0 na Azam FC kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi mwaka huu.

Kichapo hicho kwenye Kombe la Mapinduzi ni kama kilitonesha kidonda cha Simba na kuwakumbusha machungu waliyopata kutoka kwa hiyohiyo Azam FC ambayo pia iliwafunga kwa mabao 2-0 kwenye mchezo wao wa mwisho kucheza kabla Ligi Kuu haijasimamishwa kwa mwezi kupisha Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 zinazofikia tamati leo huko Morocco.

Kabla ya kupoteza mchezo dhidi ya Azam FC kwenye Ligi, Simba ilikuwa na mwenendo mzuri hapo kabla ambapo ilipata ushindi katika mechi nne mfululizo huku ikifunga mabao 11 na kuruhusu hyavu zake kutikiswa mara moja tu.

Ni mechi inayokutanisha timu mbili ambazo hazijaachana kwa tofauti kubwa ya pointi ingawa Mtibwa Sugar imecheza idadi kubwa ya mechi ambazo ni nane hadi sasa huku Simba ikicheza mechi tano tu.

Wageni Mtibwa Sugar wapo nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 10. ushindi wa leo unaweza kuwasogeza hadi katika nafasi ya nne kwenye msimamo na wataiporomosha Simba kwa nafasi moja chini.

Ni kama ilivyo kwa Simba ambayo nayo ikiibuka na ushindi leo, itafikisha pointi 15 ambazo zitaitoa katika nafasi ya tano hadi ile ya tatu.

Katika mchezo wa leo, Simba itawakosa Jonathan Sowah na Allasane Kante ambao kila mmoja ameanza kutumikia adhabu ya kukosa michezo mitano baada ya kusimamishwa kwa kosa la kucheza rafu hatarishi katika mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Azam FC.

Wakati Simba katika mechi tano zilizopita za Ligi Kuu imeshinda nne na kupoteza moja, Mtibwa Sugar yenyewe imepata ushindi katika mchezo mmoja, imetoka sare tatu na kupoteza mara moja.