Beki Yanga auona ugumu wa ligi

Muktasari:

  • Gadiel aliyesajiliwa na Yanga msimu huu akitokea Azam alisema wanatakiwa kuzidisha ushirikiano na kupambana kwa nguvu zote katika michezo yote ijayo ili kwenda sawa na kasi ya ligi.

Beki wa kushoto wa Yanga, Gadiel Michael amekiri Ligi Kuu Bara msimu huu ni ngumu wanahitaji kupambana zaidi  ili kutetea ubingwa wao.

Gadiel aliyesajiliwa na Yanga msimu huu akitokea Azam alisema wanatakiwa kuzidisha ushirikiano na kupambana kwa nguvu zote katika michezo yote ijayo ili kwenda sawa na kasi ya ligi.

"Ligi ni ngumu  na tunashukuru  mechi iliyopita na Ndanda tulishinda. Licha ya kushinda kwa bao moja, lakini muhimu ni pointi tatu kwani zimetufanya kulingana pointi na wapinzani wetu (Simba).

"Muhimu ni kuzidi kushirikiana na kuongeza juhudi ili  tuweze kupata pointi nyingine katika mchezo ujao (dhidi ya Mtibwa) Jumamosi . Kama tutaendeleza ushirikiano na kila mchezji atajitolea basi ushindi ni lazima katika mchezo huo.

"Sisi ni mabingwa watetezi na tunahitaji tena kuchukua ubingwa msimu huu hivyo hilo halitafanikiwa kama hatutaonyesha juhudi,"alisema Gadiel.

Yanga inashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi nane sawa na Simba na Prisons.