Benitez amtolea macho chipukizi wa Liverpool
Muktasari:
- Benitez anajaribu kutafuta vijana wenye kasi katika kikosi chake baada ya kurejea katika Ligi Kuu.
- Ojo (20), anaweza kuruhusiwa kuondoka Anfield msimu huu baada ya kucheza mechi moja tu msimu uliopita.
London. Kocha wa Newcastle, Rafa Benitez yupo katika mazungumzo na Liverpool kuhusu kumchukua kwa mkopo wa muda mrefu winga Sheyi Ojo.
Benitez anajaribu kutafuta vijana wenye kasi katika kikosi chake baada ya kurejea katika Ligi Kuu.
Ojo (20), anaweza kuruhusiwa kuondoka Anfield msimu huu baada ya kucheza mechi moja tu msimu uliopita.
Winga huyo pia anatakiwa na Burnley pamoja na Middlesbrough, lakini Newcastle ipo katika nafasi nzuri zaidi kumsajili, kwa mujibu wa gazeti la Independent.
Ojo alijijenga uzoefu zaidi wakati alipokuwa akicheza kwa mkopo katika klabu za Wigan na Wolves.