Boko, Okwi watajwa washambuliaji bora

DJIBOUTI. NAHODHA na straika wa Simba, John Bocco na Emmanuel Okwi raia wa Uganda, wametajwa kuwa ndiyo washambuliaji bora ndani ya kikosi chao na Mfaransa wao Pierre Lechantre amepanga kuwatumia pacha mechi ijayo.

Lechantre amesema, washambuliaji hao wanamaelewano kiuchezaji na msaada kwenye timu.

“Kwenye mechi ijayo nafikiria kuwatumia Bocco na Okwi mbele kwenye ushambuliaji kwa sababu ninachokiamini ndiyo washambuliaji bora kwenye timu,” alisema Lechantre.

Washambuliaji hao ambao ndiyo wanatikisha kwenye safu ya ushambuliaji wanaoongoza kwenye ligi kuu ambapo Okwi anaongoza.

Wachezaji hao wamekuwa na maelewano katika uchezaji tangu walipoanza kucheza pamoja mwanzoni mwa msimu huu.

Jana Jumatano Simba iliibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya Gendermarie na kuwafanya kusonga mbele kwa jumla ya mabao 5-0.