CAF yazuia watatu Yanga, yumo Djuma na Aucho

CAF yazuia watatu Yanga, yumo Djuma na Aucho

Muktasari:

  • YANGA imepokea taarifa mbaya kuelekea mchezo dhidi ya Rivers United Jumapili ikiwaambia mastaa wake watatu hawatavaa jezi katika dakika 180 za mechi hizo mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika.

YANGA imepokea taarifa mbaya kuelekea mchezo dhidi ya Rivers United Jumapili ikiwaambia mastaa wake watatu hawatavaa jezi katika dakika 180 za mechi hizo mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mastaa hao ni kiungo Khalid Aucho wa Uganda, beki Djuma Shaban na mshambuliaji Fiston Mayele wote Wakongomani.

Kuzuiwa kwa mastaa hao kunatokana na klabu ya El Makkasa ya Misri kuchelewesha hati ya uhamisho wa Kimataifa (ITC) ya Aucho kama ilivyokuwa kwa AS Vita ingawa na Yanga nao walikuwa na vimeo vyao walivyopaswa kupeleka uthibitisho kwa wakati.

Yanga kupitia Kurugenzi ya Mashindano yake ya mashindano iliomba kwa wakati uhamisho huo lakini Waarabu hao ambao awali waligoma kumwachia Aucho wakitaka aongeze mkataba ni kama walichukia kusikia kiungo huyo amesaini Yanga siku chache baada ya kuondoka nchini humo.

Kosa kama hilo lilifanyika tena nchini DR Congo na klabu za Union Maniema na AS Vita nazo hazikutuma kwa kuthibitisha kwa wakati uhamisho wa wachezaji hao.

Mwanaspoti linajua pia uwepo wa madeni mbalimbali ya wachezaji wa zamani uliisababishia Yanga kutokamilisha uhamisho huo kwa wakati na Fifa ilitaka uthibitisho wa kumalizwa kwa madeni hayo.

Fifa ilikomaa na Yanga wakibanwa na sheria mpya ya leseni za klabu ambazo kama unakesi ya madai ni vigumu kukufungulia kukamilisha sajili za wachezaji hatua ambayo Yanga ilikwepa rungu hilo dakika za mwisho.