Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chanzo kifo cha Omary Abdulkadir hiki hapa

Refa mstaafu na Mwenyekiti wa Chama cha Marefa wa Soka Tanzania (Frat), Omary Abdulkadir enzi za uhai wake. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Abdulkadir ni miongoni mwa marefa watatu wa Tanzania waliowahi kuchezesha fainali za Afcon wengine wakiwa ni marehemu Hafidh Ally Tahir na Frank Komba.

Dar es Salaam. Familia ya refa mstaafu na Mwenyekiti wa Chama cha Marefa wa Soka Tanzania (Frat), Omary Abdulkadir imetaja sababu ya kifo cha mkufunzi huyo wa marefa wa Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kilichotokea usiku wa kuamkia leo kuwa ni maradhi ya figo.

Abdulkadir anazikwa leo Septemba 13 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam ambapo mtoto wake, Ahmed Omary amesema kuwa umauti ulimfika akiwa anapambana na maradhi hayo.

Ahmed Omary amesema kuwa msiba huo umeacha pigo kubwa kwao.

“Mzee alikuwa anaugua kwa muda mrefu maradhi ya figo. Kuna nyakati alipata changamoto kama vile presha lakini hasa kilichokuwa kinamsumbua ni figo. Sisi kama wanafamilia tumepata pigo kubwa sana maana mzee alikuwa ni mtu wa watu, mwenye upendo na muhimili.”

“Hata hivyo Mungu amempenda zaidi hatuna namna inabidi tukubali hili na tulipokee. Tunatoa shukrani zetu kwa wote walioshirikiana nasi kuanzia katika kumuuguza mzee wetu hadi sasa,” amesema Ahmed.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemuelezea Abdulkadir kama miongoni mwa watu waliotoa mchango mkubwa kwa soka la Tanzania.

“Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ampokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu (FRAT), Omary Abdurkadir.

"Ametuma salamu za pole kwa, familia, dugu, jamaa, marafiki, Frat, wanafamilia wa mpira wa miguu na wote walioguswa na msiba huo. Rais Karia amesema mchango wa Abdulkadir katika maendeleo ya mpira wa miguu kwenye eneo la waamuzi utakumbukwa daima.”

“Wakati wa uhai wake, Abdurkadir alikuwa mwamuzi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa) kabla ya kustafu, alikuwa mkufunzi wa waamuzi na mpaka mauti yanamkuta alikuwa mwenyekiti wa FRAT. Mungu allaze roho ya marehemu mahala pema peponi, Amina,” imesema taarifa hiyo ya TFF.

Taarifa ya Frat imesema mchango wa Abdulkadir katika urefa wa soka hautosahaulika.

“Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu FRAT, Emmanuel Chaula kwa masikitiko makubwa amepokea taarifa za msiba wa Mwenyekiti wa chama cha Waamuzi Omary Abdurkadir.

"Ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa, waamuzi, wanafamilia wa mpira wa miguu na wote walioguswa na msiba huo.”

"Abdurkadir alikuwa mwamuzi mstaafu wa FIFA Na Mkufunzi wa Waamuzi Chaula amesema Abdurkadir alikuwa na mchango mkubwa sana katika maendeleo ya waamuzi wa Mpira wa Miguu hapa nchini. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, Ameen,” imeeleza taarifa ya Frat.

Abdulkadir anakumbukwa kwa kuwa refa wa pili wa Tanzania kuchezesha fainali za mataifa ya Afrika (Afcon) ambapo alifanya hivyo mwaka 2000 wakati fainali hizo zilipofanyika Ghana na Nigeria.

Katika fainali hizo, Abdulkadir alichezesha mechi moja tu ambayo ilikuwa ni ya hatua ya makundi ambayo Algeria ilipata ushindi wa mabao 3-1.

Kwenye mechi hiyo, Abdulkadir alimtoa kwa kadi nyekundu katika dakika za mwanzoni, mchezaji Eric Engo wa Gabon jambo ambalo lilikuwa gumzo.