Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dembele aingia kwenye historia Kombe la Dunia

DEMBELE Pict

Muktasari:

  • Hat-trick hiyo imemfanya mshambuliaji huyo wa Paris Saint-Germain kuwa mchezaji wa pili kufunga mabao matatu kwa haraka zaidi tangu kuanza kwa mchezo katika historia ya Kombe la Dunia.

Nyota wa Ufaransa, Ousmane Dembele, ameandika historia mpya usiku wa kuamkia leo, Jumamosi katika Kombe la Dunia 2026 baada ya kufunga hat-trick ndani ya dakika 32 katika ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Norway.

Hat-trick hiyo imemfanya mshambuliaji huyo wa Paris Saint-Germain kuwa mchezaji wa pili kufunga mabao matatu kwa haraka zaidi tangu kuanza kwa mchezo katika historia ya Kombe la Dunia.

Dembele aliingia kwenye michuano hiyo akiwa katika kiwango cha juu kufuatia kutwaa tuzo ya Ballon d'Or mwaka jana na kuisaidia PSG kutwaa taji la pili mfululizo la Ligi ya Mabingwa Ulaya, kiwango ambacho ameendelea kukionyesha akiwa na kikosi cha Didier Deschamps.

DEMBE 01

Aliifungia Ufaransa bao la kwanza dakika ya saba baada ya kupokea pasi ndefu kutoka kwa Kylian Mbappe, akawakwepa mabeki wawili wa Norway kabla ya kumalizia kwa utulivu.

Dakika ya 20 aliongeza bao la pili kwa staili iliyofanana, akitokea upande wa kulia, kukata kuelekea katikati na kuachia shuti la mguu wa kushoto lililojaa wavuni.

Hat-trick yake ilikamilika dakika ya 32 baada ya Michael Olise kuvuruga safu ya ulinzi wa Norway kabla ya  Dembele kufunga bao lake  la tatu.

DEMBE 02

Licha ya ushindi huo mnono, Dembele alikosa kuivunja rekodi ya Erich Probst wa Austria, ambaye bado anashikilia rekodi ya kufunga hat-trick ya mapema zaidi katika Kombe la Dunia baada ya kufunga mabao matatu ndani ya dakika 24 dhidi ya Czechoslovakia mwaka 1954.

Nafasi ya tatu kwenye orodha hiyo inashikiliwa na Gary Lineker wa England aliyefunga hat-trick ndani ya dakika 36 dhidi ya Poland mwaka 1986 huku nguli wa Ujerumani Magharibi, Gerd Muller, akifuatia baada ya kufunga ndani ya dakika 38 dhidi ya Peru mwaka 1970.

Hata hivyo, rekodi ya kufunga hat-trick kwa muda mfupi zaidi kati ya bao la kwanza na la tatu bado inamilikiwa na Laszlo Kiss wa Hungary, aliyefunga mabao matatu ndani ya dakika saba mwaka 1982 baada ya kuingia akitokea benchi dhidi ya El Salvador.