Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diarra sasa aifuata Senegal

Muktasari:

  • Kocha wa Mali, Tom Saintfiet, amewamwagia sifa wachezaji kwa namna alivyoweza kujidhibiti na kubaki mtulivu licha ya changamoto ya kucheza wakiwa pungufu ya mchezaji mmoja.

Casablanca, Morocco. Kipa namba moja wa Yanga, Diarra Djigui usiku wa juzi alikuwa shujaa wa timu ya taifa ya Mali, baada ya kuokoa penalti mbili na kuivusha kimiujiza timu hiyo kucheza robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 ikiifuata Senegal iliyotangulia mapema kwa kuifumua Sudan kwa mabao 3-1.

Diarra aliyetumika katika mechi zote tatu za makundi za michuano hiyo ya 35, juzi usiku katika mechi ya 16 Bora dhidi ya Tunisia aliokoa penalti mbili baada ya dakika 120 kushuhudiwa timu hizo zikifunga bao 1-1, Mali ikipata bao la kusawazisha dakika za majeruhi za muda wa kawaida wa dakika 90, huku ikiwa pungufu ya mchezaji mmoja.

Kipa huyo tegemeo wa Yanga, ndiye aliyechaguliwa pia kuwa nyota wa mchezo (Man of the Match) kwa kazi nzuri aliyoifanya akiiwezesha timu hiyo kufikisha mechi nne mfululizo za michuano hiyo bila kupoteza kwani katika hatua ya makundi ikiwa Kundi A sambamba na wenyeji Morocco, ilitoka sare tatu.

Katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mohamed V, jijini Casablanca, Mali ilionyesha uimara na utulivu wa hali ya juu licha ya kuwa pungufu ya mchezaji mmoja baada ya Woyo Coulibaly kupewa kadi nyekundu dakika ya 26 kwa kumkanyaga Hannibal Mejbri.

Kadi hiyo imemfanya nyota huyo wa zamani Leicester City anayekipiga kwa sasa Sassuolo ya Italia kuwa mchezaji wa nne wa Mali kulimwa kadi nyekundu katika michuano hiyo iliyoanza Desemba 21 mwaka jana itakayomalizika Januari 18 kabla ya Tunisia kupata bao la kuongoza dakika ya 88 kupitia Firas Chaouat aliyemalizia kwa kichwa pasi ya Elias Saad, mpira uliopita kirahisi kipa Diarra.

Hata hivyo dakika za majeruhi  Yassine Meriah wa Tunisia alionekana kuucheza mpira kwa mkono na kusababisha penalti iliyowekwa kimiani na Lassine Sinayoko na kusababisha pambano kwenda muda wa nyongeza wa dakika 30 na Diarra na wenzake kupambana wakiwa pungufu kwa kuibana Tunisia hadi katika penalti na kushinda 3-2.

Kocha wa Mali, Tom Saintfiet, amewamwagia sifa wachezaji kwa namna alivyoweza kujidhibiti na kubaki mtulivu licha ya changamoto ya kucheza wakiwa pungufu ya mchezaji mmoja.

“Ninajivunia golikipa na wachezaji wote,” alisema Saintfiet.

“Kabla ya mechi, niliwaambia kuwa wao ni mabingwa. Kama tungecheza na wachezaji 11, huenda tungepata faida zaidi.” Aliongeza:

“Tutakutana na Senegal katika robo fainali. Senegal wanaopewa nafasi kubwa kama ambavyo Morocco na Tunisia walivyokuwa katika mechi zetu zilizopita. Tuna lengo, ambalo ni kuendelea kubaki kwenye mashindano.”