Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Donnarumma kuondoka PSG, Chelsea, Man United zatajwa

Muktasari:

  • Chelsea na Manchester United vimeripotiwa kuulizia upatikanaji wake ndani ya saa chache zilizopita.

Kipa wa kimataifa wa Italia, Gianluigi Donnarumma, anatarajiwa kuondoka Paris Saint-Germain (PSG) msimu huu wa kiangazi baada ya kuachwa nje ya kikosi kilichocheza fainali ya UEFA Super Cup dhidi ya Tottenham, hatua inayodhihirisha kuvunjika kwa uhusiano wake na mabingwa hao wa Ulaya.

Kwa mujibu wa ripoti za Fabrizio Romano, Donnarumma, 26, hatasaini mkataba mpya Parc des Princes na kuondoka kwake msimu huu ni jambo linalotarajiwa zaidi. PSG wanapanga kumuuza sasa ili kuepuka kumpoteza bure mwishoni mwa msimu, kwani mkataba wake unamalizika 2026.

RMC Sport imeeleza kuwa kipa huyo atakubali kuondoka msimu huu endapo atapata mradi wa soka unaomvutia, vinginevyo atabaki PSG hadi mkataba wake utakapokamilika.

Vilabu viwili vya Ligi Kuu England, Chelsea na Manchester United vimeripotiwa kuulizia upatikanaji wake ndani ya saa chache zilizopita, ingawa hakuna ofa rasmi iliyowasilishwa.

Manchester United kwa sasa wanamtegemea Andre Onana kama kipa namba moja, lakini makosa ya mara kwa mara yameibua mashaka juu ya mustakabali wake. Chelsea, ambao wameshakubaliana na kuondoka kwa Djordje Petrovic na Kepa Arrizabalaga, wanajiandaa kuanza msimu na Robert Sanchez kama kipa namba moja, lakini naye pia amekuwa na makosa ya mara kwa mara.

Chelsea watafungua msimu kwa mchezo wa London Derby dhidi ya Crystal Palace Agosti 17, huku Manchester United wakipambana na Arsenal siku hiyo hiyo.