Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DR Congo yaanza na sare kwa Ureno, Ronaldo akifichwa

Muktasari:

  • Dakika sita tu zilitosha kwa Ureno kutangulia kupata bao likifungwa kwa kichwa na Joao Neves akimalizia krosi safi ya Pedro Neto kutoka pembeni kushoto.

DR Congo imeukataa unyonge kwa kulazimisha sare 1-1 na Ureno  yenye mastaa wakubwa duniani akiwemo Cristiano Ronaldo.

Dakika sita tu zilitosha kwa Ureno kutangulia kupata bao likifungwa kwa kichwa na Joao Neves akimalizia krosi safi ya Pedro Neto kutoka pembeni kushoto.

Ureno hata kabla na baada ya bao hilo ilitawala vizuri mchezo huo ikijenga mashambulizi yake mengi makali kutoka pembeni baada ya kushtukia hesabu za Wakongomani ambao walijikita kujilinda zaidi.

Baada ya kuruhusu bao hilo DR Congo  ikajiongeza kwa kufanya mashambulizi ya kushtukiza mara baada ya Ureno kupoteza mpira, ikitumia mabeki wake wa pembeni na viungo.

DR Congo ikafanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 45+5 kupitia Yoane Wissa kwa kichwa akiunganisha krosi ya beki   Arthur Masuaku.

Timu hizo zikaenda mapumziko zikiwa zimefungana kwa bao 1-1, mabao yote yakiwa ya aina moja kwa mashambulizi ya kutokea pembeni.

Kipindi cha pili timu zote ziliendelea kutengeneza mashambulizi makali lakini uimara wa safu za ulinzi,yakashindwa kuzalisha mabao.

Dakika ya 55 Ureno ilikaribia kupata bao baada ya kiungo wake Joao Conceicao kufunga lakini likakataliwa, baada ya kunaswa na mtego wa kuotea.

Staa wa Ureno na nahodha wa timu hiyo Cristiano Ronaldo hakuweza kuonyesha makeke yake baada ya kubanwa vizuri ambapo mashuti yake mawili yakashindwa hata kulenga lango akitoka kwenye mchezo huo bila hata shuti moja lililolenga lango.

Viungo wengine hatari wa Ureno, Vitinha na Bruno Fernandes nao walikumbana na wakati mgumu wakishindwa kuonyesha uwezo wao bora ambapo nahodha huyo wa Manchester United naye akamaliza dakika 90 kwa kupiga shuti moja pekee ambalo nalo halikulenga lango.

Mpaka mwisho wa mchezo huo wa kwanza wa Kundi A ukamalizika kwa timu hizo kufungana kwa bao 1-1.