Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Euro sasa imefikia patamu

Munich, Ujerumani. Michuano ya Euro imefikia patamu, ambapo sasa kila timu ukiondoa zile za kundi A, nyingine zote zimebakisha mechi moja ili kumaliza hatua ya makundi.

Hadi sasa timu zilizofanikiwa kufuzu ni tatu tu ya kwanza ikiwa ni mwenyeji Ujerumani ikifuatiwa na Hispania na Ureno ambazo zimeshinda mechi zao mbili za kwanza za makundi.

Katika mechi za mwisho za makundi zinatafutwa timu 13 ambazo zitaungana na hizi tatu kwa ajili ya kupambana katika hatua ya 16 bora.

Katika kundi A, ambapo Ujerumani tayari imeshafuzu timu inayoonekana kuwa na nafasi ya kumfuata ni Uswis lakini hiyo itaamuliwa na matokeo yao ya leo katika mchezo wao mwisho dhidi ya Ujerumani.

Kundi B, ambalo Hispania imeshafuzu kwa alama zao sita, timu inayoshika nafasi ya pili kwa pointi tatu ni Italia ambayo imeshinda mechi moja na kupoteza moja.

Mechi za mwisho za kundi hili zinachezwa kesho na Italia inahitaji ushindi dhidi ya Croatia inayoburuza mkia ili kusonga mbele ama itoke sare na iombee Albania yenye pointi moja  ipoteze au itoe sare mbele ya Hispania.

Kundi hili linaonekana kuwa gumu kwani yoyote atakayeanguka katika mchezo wa mwisho anaweza kujikuta mkiani mwa msimamo.

Kwa upande wa kundi C ambalo England ndio vinara kwa alama zao nne ilizopata baada ya kushinda mechi moja na sare moja, hakuna timu yenye uhakika wa kufuzu hadi sasa.

England itahitaji sare au kushinda mchezo wao wa mwisho dhidi ya Slovenia ili kufuzu wakati Denmark inayoshikilia nafasi ya pili ikitakiwa kushinda dhidi ya Serbia ili kufuzu.

Serbia ambayo inaburuza mkia kwa pointi yao moja inaweza kwenda hatua inayofuata ikiwa itashinda mchezo wa mwisho mbele ya Denmark kisha Slovenia ikafunga ama kutoka sare dhidi ya England. Mechi za mwisho za kundi hili zitapigwa kesho.

Kundi la Kylian Mbappe na Ufaransa yake nalo limekaa kimtego, hadi sasa Uholanzi ndio inaongoza kundi D ikiwa na pointi nne sawa na zile za Ufaransa lakini wao wapo juu kwa sababu wamefunga mabao mengi(mawili), wakati Ufaransa ikiwa imefunga moja tu.

Timu inayoshika nafasi ya tatu ni Austria ambayo ina pointi tatu wakati Poland ikiwa na inaburuza mkia bila pointi.

Ufaransa na Uholanzi zinahitaji kushinda mechi zao za mwisho ama kutoa sare tu ili kwenda hatua inayofuata wakati Austria inahitaji ushindi.

Mechi zao zitapigwa keshokutwa, na Uholanzi itakutana na Austria wakati Ufaransa ikimenyana na vibonde Poland.

Moto utawaka zaidi kundi, E. Hadi sasa timu zote zimeshinda mechi moja moja kati ya mbili na zote zina pointi tatu. Kinara wa kundi ni Romania, ikifuatiwa na Ubelgiji, Slovakia na Ukraine.

Ili kwenda hatua inayofuata katika mechi za mwisho zitakazokutanisha timu zote hizo, ile itakayoshinda ndio itasonga.
Ikiwa mechi hizo pia zitamalizika kwa sare basi kanuni zitatumika kuamua nani amalize nafasi ya kwanza na ya mwisho.

Katika kundi F ambalo Ureno imeshafuzu baada ya kushinda mechi mbili, Uturuki inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi tatu.

Katika mechi za mwisho Uturuki itaumana na Jamhuri ya Czech na ili kufuzu itatakiwa kushinda ama kutoa sare lakini muda huohuo ikiiombea mabaya Georgia ipoteze dhidi ya Ureno.

Ikiwa Uturuki itapata sare kisha Georgia ikashinda, mambo yanaweza kubadilika kwa kutazama mabao ya kufunga na kufugwa.

Mbali ya kumaliza nafasi ya kwanza na ya pili bado timu zinaweza kuingia hatua ya 16 bora kwa kumaliza nafasi ya tatu kwa pointi nyingi best looser.

Hapa zinahitaji timu nne ambazo zitamaliza nafasi ya tatu kwa pointi nyingi zaidi.

Hadi sasa timu zenye nafasi kubwa ya kupita hapo ni Austria, Slovakia, Slovenia na Albania.