Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

FIFA yamchunguza Refa Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Katika mechi hiyo ya kundi E, Ujerumani iliyoshinda mabao 7-1, Shaun alikuwa chumba cha waamuzi wa msaada wa Video yaani (VAR), ambapo alionekana kutumia kidole gumba na kidole cha shahada kuunda ishara inayofanana na 'OK' iliyogeuzwa chini.

Shirikisho la Soka la Duniani (FIFA), limeanza uchunguzi wa mwamuzi kutoka Australia, Shaun Evans baada ya kuonyesha ishara inayoashiria kuunga mkono itikadi ya watu weupe, katika mechi ya Kombe la Dunia kati ya Ujerumani na Curacao.

Katika mechi hiyo ya kundi E, Ujerumani iliyoshinda mabao 7-1, Shaun alikuwa chumba cha waamuzi wa msaada wa Video yaani (VAR), ambapo alionekana kutumia kidole gumba na kidole cha shahada kuunda ishara inayofanana na 'OK' iliyogeuzwa chini.

Ishara hiyo imeibua mjadala mkubwa ambapo inadaiwa hutumika kama alama ya makundi ya siasa zenye mrengo mkali wa kulia, japo mara nyingi imekuwa ikitumika kawaida kuonyesha kuridhika au kukubali, jambo ambalo FIFA imeanza kwa kulichunguza.

Evans ambaye ni mwamuzi kutoka Ligi Kuu ya Australia (A-League Men), aliyechaguliwa na FIFA, alionekana amesimama wakati wa kupiga picha akionyesha ishara iliyoibuka sintofahamu, akiwa na wenzake, Hamza El Fario na msaidizi, Nicolas Gallo.

Mwamuzi kutoka Australia, Shaun Evans (aliyesimama kushoto)

Katika picha hiyo, Evans alisimama nyuma ya Hamza El Fario na msaidizi Nicolas Gallo na alionyesha tabasamu alipofanya ishara hiyo kabla ya kugeuka na kuondoka, jambo lililoibua mjadala na kuifanya FIFA kuanza uchunguzi wa tukio hilo.

Ishara hiyo iliwahi kufanywa na mkandarasi (subcontractor) aliyefanya kazi na huduma za matangazo wakati wa mashindano ya Olimpiki, Paris Ufaransa mwaka 2024, ambaye alionyesha ishara ya mkoano inayofanana na 'OK', ikiwa imegeuzwa chini.

Katika fainali hizo za Skateboarding ya Wanawake wa Mitaani, mkandarasi huyo alitambuliwa na mamlaka zinazohusika na matangazo ya Olimpiki, hasa Olympic Broadcasting Services, ambapo alifutiwa kibali chake cha kuingia (accreditation).

Kufutwa kwa kibali cha ofisa huyo katika fainali za Olimpiki zilihitimisha kuendelea na majukumu yake katika mashindano hayo, kwani tabia hiyo iliyorekodiwa ilitafsiriwa kama ishara isiyofaa katika mazingira ya tukio hilo la kimataifa.

Mwamuzi kutoka Australia, Shaun Evans (aliyesimama kushoto)

Anti-Defamation League (ADL) ambalo ni shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa nchini Marekani mwaka 1913, linasema matumizi mengi ya ishara hiyo ni kuonyesha kuridhika au kuunga mkono kwa jambo, hivyo, ni muhimu kuongeza zaidi umakini.

Shirika hilo lililoanzishwa kwa ajili ya kupambana na ubaguzi wa rangi, dini, na chuki dhidi ya makundi mbalimbali na

Kulinda haki za kiraia na usawa wa kijamii, lilidai ishara hiyo ya picha ni mbinu ya watu wanaoegemea mrengo wa kulia.

Shirika hilo linadai watu wengi wanaopiga picha na kuweka mitandaoni wakiwa na mrengo wa kulia maana yake huashiria fikra za uhifadhi wa mila za maeneo yao wanayotoka au wanayoishi, ikihusiha mfumo wa kawaida au sera za kihafidhina.