Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

FIFA yampa Kizuguto mechi za lawama

Muktasari:

  • Timu tisa (9) za Afrika zimefuzu moja kwa moja katika Fainali za Kombe la Dunia 2026 zitakazofanyika Marekani, Canada na Mexico mwakani.

Dar es Salaam. Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) limemteua Mtanzania, Baraka Kizuguto kuwa Mratibu Mkuu wa mechi za mchujo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026 kwa kanda ya Afrika ambazo zitafanyika Morocco, Novemba 23 na Novemba 16 mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imefafanua kuwa Kizuguto atasimamia mechi moja ya nusu fainali na mchezo wa fainali.

"Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) limemteua Meneja Mashindano wa TFF, Baraka Kizuguto kuwa Mratibu (General Coordinator) wa michezo ya nusu fainal ya hatua za awali kufuzu Kombe la Dunia Kanda ya Afrika (Play-Off Tournament) kati ya Nigeria vs Gabon na fainali. Michezo hiyo itachezwa Rabat, Morocco Novemba 13 na Novemba 16, 2025," imefafanua TFF.

Mshindi wa mchezo baina ya Gabon na Nigeria ataingia hatua ya fainali ya mashindano hayo ambapo atakutana na mshindi wa mchezo baina ya Cameroon na DR Congo.

Timu itakayoibuka na ushindi katika hatua ya fainali, itapata fursa ya kucheza hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia ambapo itakabiliana na timu kutoka kanda nyingine ya soka.

Timu zinazocheza mechi hizo za mchujo kwa Kanda ya Afrika ni zile ambazo zilimaliza katika nafasi ya pili kwenye makundi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia kwa upande wa Afrika.

DR Congo ilimaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi B huku Cameroon ikimaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi D.

Nigeria ilishika nafasi ya tatu katika msimamo wa kundi C na Gabon ilimaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi F.