Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fountain Gate, Mbeya City zakataa unyonge Yanga, Simba

Muktasari:

  • Yanga inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 10 huku Simba ikishika nafasi ya saba ikiwa na pointi tisa.

Timu za Fountain Gate na Mbeya City, zimetamba kwamba zimejipanga kuvuna pointi tatu katika mechi dhidi ya Yanga na Simba kesho Alhamisi katika viwanja tofauti, zikiwa za muendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika Uwanja wa KMC, Dar es Salaam, Yanga itaikaribisha Fountain Gate kuanzia saa 10:00 jioni na Simba itaialika Mbeya City katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam kuanzia saa 1:00 usiku.

Kocha wa Fountain Gate, Mohammed Laizer amesema kuwa pamoja na ubora wa Yanga, wao wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi.

"Tuko tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Yanga. Maandalizi yanaenda vizuri. Tunajua tunakutana na Yanga ambayo ni timu bora. Tunawaheshimu Yanga ni timu nzuri lakini sisi tumekuja kushindana ili kupata matokeo mazuri," amesema Laizer.

Kaimu Kocha Mkuu wa Mbeya City, Patrick Mwangata amesema kuwa pamoja na mwenendo wao usioridhisha, watahakikisha wanaondoka na furaha dhidi ya Simba.

"Tunajua kwetu ni mchezo mgumu sana kwa sababu tumetoka kupotez mechi tatu mfululizo. Tunawaheshimu lakini sisi kama Mbeya City tumejiandaa vizuri kuhakikisha mchezo wa kesho, tunafanya vizuri," amesema Mwangata.

Wakati wapinzani wao wakitamba, Yanga na Simba zenyewe nazo zimesisitiza kwamba malengo yao ni kupata ushindi kesho.

Kocha Mkuu wa Yanga, Pedro Goncalves amesema kuwa wamejipanga kwa ajili ya mchezo huo.

"Tunafahamu kuwa wapinzani wetu wamejiandaa vizuri pia. Tunahehsimu kila mpinzani anayekuja mbele yetu. Tutacheza kama vile tunacheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa. Falsafa yetu haitabadilika. Dhamira yetu ni ushindi tu,” amesema Goncalves.

Kocha wa Simba, Selemani Matola alisema,"kwenye ligi hakuna timu nyepesi. Mbali ya ugumu huo tumejipanga na kufanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya kushinda na kupata pointi tatu kwenye mchezo wa kesho.”