Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huyu ndio ‘Super Sub’ Thalente Mbatha

Muktasari:

  • Mbatha alijiunga na Orlando Pirates, Januari mwaka huu akitokea Supersport United.

Dar es Salaam. Thalente Mbatha halikuwa jina kubwa katika kikosi cha Afrika Kusini kabla ya raundi mbili za mwanzo za kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (Afcon) 2025 dhidi ya Uganda na Sudan Kusini.

Hata hivyo baada ya mechi hizo, nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 anayechezea Orlando Pirates amegeuka kuwa gumzo nchini Afrika Kusini.

Umaarufu wa Mbatha umetokana na jinsi alivyoiokoa Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ katika mechi hizo mbili kwa kuifungia mabao ya dakika za jioni ambayo yameiwezesha kumaliza na pointi nne katika mechi hizo.

Jambo la kushangaza kwa nyota huyo ni kwamba mechi zote hizo alizofunga mabao hayo, amefanya hivyo akitokea benchi.

Katika mchezo wa leo dhidi ya Sudan Kusini, Mbatha alifunga bao la ushindi katika dakika za nyongea wakati timu yake iliposhinda mabao 3-2.

Mbatha katika mechi ya leo ambayo Afrika Kusini ilikuwa ugenini huko Juba, Sudan Kusini, aliingia katika dakika ya 72 kuchukua nafasi ya Sphephelo Sithole.

Mechi hiyo ilionekana ingemalizika kwa sare ya mabao 2-2 kama sio bao la ushindi la Mbatha, kabla ya hapo Sudan Kusini ikifunga mabao yake kupitia kwa Tito Okello na Valentino Kuach Yuel huku mawili ya Afrika Kusini yakipachikwa na Oswin Apollis.

Kabla ya mchezo wa leo, Mbatha aliinusuru Afrika Kusini isipokee kichapo nyunbani kutoka kwa Uganda baada ya kuisawazishia katika dakika za nyongeza kwenye mechi iliyochezwa Ijumaa iliyopita, Septemba 6 na kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Katika mechi hiyo dhidi ya Uganda, Mbatha aliingia akitokea benchi katika dakika ya 81 akichukua nafasi ya Sithole.

Kabla ya hapo, Uganda ilifunga mabao mawili kupitia kwa Denis Omedi na Rogers Mato huku bao la kwanza la Afrika Kusini likiwekwa kimiani na Lyle Foster.

Ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Sudan Kusini leo umeifanya Afrika Kusini kukaa katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi K ikiwa na pointi nne sawa na Uganda ambayo inaongoza.

Hata hivyo Uganda iko juu ya Afrika Kusini kwa vile ina utofauti mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Nafasi ya tatu ya kundi hilo inashikwa na Congo na Sudan Kusini inashika mkia.