Karia aikataa Simba

Karia aikataa Simba

Muktasari:

  • RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amefunguka tuhuma zinazoenezwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa yeye ni shabiki na mwanachama wa klabu ya Simba, akisema "Sio kweli, mimi ni Coastal Union."

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amefunguka tuhuma zinazoenezwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa yeye ni shabiki na mwanachama wa klabu ya Simba, akisema "Sio kweli, mimi ni Coastal Union."

Karia amekanusha tuhuma hizo leo kwenye mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao kupitia zoom kujadili tathmini na matarajio ya wadau wa soka juu ya mwenendo wa usajili wa wachezaji kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya NBC 2022/2023.

Akizungumza hayo Karia alisema huu ni mpira wa miguu na unaongoza na viongozi ambao wametoka kwenye mpira, wana klabu zao na hivyo ni lazima wawe na timu zao wanazoshabikia kutokana na mapenzi yao kwani asingekuwa shabiki wa Boxing kwa sababu hauongozi.

Karia aliongeza licha ya yote ila jambo la msingi linalotakiwa ni kufuata kanuni za maadili ili kuhakikisha kiwango hicho ni kikubwa zaidi cha kutenda haki.

Kuhusu Shirikisho hilo pia kuwa na mashabiki wengi wa Simba, Karia alisema hana uhakika kama liko hivyo ila amewataka mashabiki kufanya tathimini huku akikiri yeye kwa upande wake sio shabiki wa timu hiyo bali ni Coastal Union kutokana na kuwahi kuingoza.

Suala la kuvaa jezi kwenye mkutano wa Simba uliofanyika miaka ya nyuma wakati akiwa Makamu wa Rais alisema kwamba aliagizwa na aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi aende akamuwakilishe kwenye kilele cha tamasha la 'Simba Day'.

Alisema wakati wa tamasha hilo alivaa jezi nyeusi lakini akapewa jezi nyekundu hivyo akaamua kuvaa kutokana na kutumwa kuwakilisha taasisi na asingeweza kuikataa