Karia ashinda urais TFF kwa asilimia 100
Tanga. Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF, wamemuidhinisha Wallace Karia kuendelea kuwa Rais wa Shirikisho hilo kwa miaka mingine minne.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Kiomoni Kibamba ametangaza hilo muda mfupi baada ya wajumbe wote wa mkutano huo kumuidhinisha.
“Mkutano mkuu huu leo hii na mahala hapa na muda huu wamemuidhinisha Wallace Karia kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu kwa miaka mingine minne,” amesema Kibamba.