Kigogo Gwambina aachia ngazi

Wednesday June 09 2021
gwambiona pic
By Saddam Sadick

Mwenyekiti wa Gwambina FC, Omary Mmasi amejiuzuru nafasi hiyo huku ikiwa haijatajwa sababu za kiongozi huyo kung'atuka.

Ikumbukwe Gwambina ambayo inashiriki Ligi Kuu kwa msimu wake wa kwanza inahaha sana kukwepa rungu la kushuka daraja kwani hadi sasa imekusanya pointi 31 na kukaa nafasi ya 17.

Afisa habari wa timu hiyo, Felician Mwenzi, amethibitisha uongozi kupokea taarifa hiyo huku akisema ni masikitiko makubwa ikizingatiwa timu haipo sehemu salama.

"Ni kweli tumepata taarifa hizo lakini ni masikitiko kwani tupo katika mapambano makali kwa kipindi hiki kigumu tukisaka matokeo mazuri" amesema Mwenzi.

Advertisement