Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kinda Brighton awindwa Man United

Manchester United wameanza mazungumzo na Brighton kwa nia ya kumsajili kiungo chipukizi Carlos Baleba, mwenye umri wa miaka 21, katika dili linaloweza kugharimu hadi pauni milioni 100 (Sh.334 bilioni)

Baleba, ambaye alijiunga na Brighton mwaka 2023 akitokea Lille ya Ufaransa, amekuwa mhimili wa kikosi hicho msimu uliopita, akicheza mechi 34 na kusaidia kumaliza nafasi ya nane. Anaweza kuungana na wenzake wa timu ya taifa ya Cameroon, kipa Andre Onana na nyota mpya Bryan Mbeumo, pamoja na Leny Yoro aliyecheza naye Lille.

Akiwa mzaliwa wa Douala, nyumbani pia kwa gwiji Samuel Eto’o, Baleba amekuwa na ndoto kubwa akimtaja Paul Pogba kama mmoja wa wachezaji waliomvutia na akisema ana malengo ya kushinda Ballon d’Or kama Rodri. Baba yake, Eugene Baleba, ndiye alimjenga akiwa na umri wa miaka 10 kwa mazoezi magumu ya mbio na mazoezi ya kuruka juu ya matairi, yaliyomsaidia hata kwenye mbwembwe zake za kusherehekea mabao.

Baada ya kuibukia akademi ya des Brasseries iliyopo Cameroon, Baleba alihamia Lille 2022 na kisha Brighton 2023 kuchukua nafasi ya Moises Caicedo. Alianza kwa changamoto kwenye kasi ya Ligi Kuu England, akifanya makosa matano yaliyopelekea mabao, lakini chini ya kocha mpya Fabian Hurzeler ameimarika na kuwa mhimili wa safu ya kiungo.

United wanaona atakuwa mshirika bora wa Bruno Fernandes wakichanganya nguvu, ukabaji mkali na uwezo wa kushika mpira sehemu ngumu tofauti na Manuel Ugarte na Casemiro ambao wamekosa ubora kwenye pasi. Amorim anaamini Baleba anaweza kuondoa mapungufu hayo, hasa kwenye mechi ambazo United inahitaji kumiliki mpira.

Licha ya kufunga mabao matatu tu msimu uliopita, Baleba ni tishio hasa kufunga mabao ya mbali akishinda tuzo ya bao bora la Aprili dhidi ya West Ham ambalo alifunga kwa shuti la mbali.

Brighton hawana haraka ya kumuuza, kwani ana mkataba hadi 2028 na chaguo la kuongeza mwaka mmoja zaidi. Lakini mradi mpya wa Amorim, pamoja na ujio wa Mbeumo, Cunha na huenda Sesko, unaweza kumvutia kuhamia Old Trafford.