Klopp:Tumecheza chini ya kiwango

Wednesday April 07 2021
madridpic

MADRID, HISPANIA. KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema vijana wake walionyesha kiwango dhaifu kwenye mchezo wao wa robo fainali ya kwanza ya  Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid jambo lililopeleka kupata kipigo cha mabao  3-1.
Mjerumani huyo alisema, "Ikiwa unahitaji  kwenda hatua ya nusu fainali kuna jambo muhimu ambalo unapaswa kufanya, lakini sisi hatukulifanya usiku wa leo (jana). Hatukucheza soka safi kiasi cha kuifanya Real Madrid kutushambulia.
Katika mchezo huo  uliofanyika  kwenye uwanja wa Alfredo Di Stefano  mchezaji wa Real Madrid,Vinicius Junior   alionekana kuwa mwiba mkali kwa Liverpool.
Vinicius alitupia mabao mawili na Marco Asensio akitupia moja huku bao la kufutia machozi la Liverpool  likifungwa na Mohamed Salah.
Liverpool ina mlima mrefu wa kupanda katika mchezo wa marudiano utakaofanyika Anfield Aprili 14 wakitakiwa kupata ushindi wa mabao 2-0 au zaidi ili kutinga hatua ya nusu fainali.
Wakati Liverpool ikikumbana na kipigo hicho cha mabao 3-1 wakiwa ugenini, Manchester City ilianza vizuri robo fainali ya kwanza kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Borussia Dortmund  ya Ujerumani ,mabao ya washindi yalifungwa na  Kevin De Bruyne na Phil Foden

Advertisement