Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Yanga aoa mke wa tatu

KOCHA wa Yanga, Luc Eymael(61) amelithibitishia Mwanaspoti kwamba anaondoka leo Ijumaa kwenda kwao Ubelgiji na atafunga ndoa Jumamosi ya Machi 28 kule Ubelgiji.

Amefafanua anayemuoa sasa ni mke wake wa tatu na kwamba tayari alishakua nao wengine wawili awali lakini akaachana nao kutokana na sababu za kawaida za kibinadamu.

Kocha huyo alisema kwamba ana watoto wawili wote wa kike aliozaa na wake wa awali na pia ana wajukuu wawili. Mtoto wake wa kwanza ana umri wa miaka 33 sawa na namba ya jezi ya besti yake mkubwa, Bernard Morrison.

“Nitaoa tena tarehe 28, huyu ni mke wa tatu baada ya kuachana na wale wawili wa kwanza,”alisisitiza.

MTEGO WA MOLINGA NA YONDANI

Straika mwilinyuma wa Yanga, David Molinga na beki Lamine Moro juzi waliwasilisha barua zao za utetezi klabuni lakini mastaa wengine watatu akiwemo Kelvin Yondani nao wamenasa kwenye mtego huo.

Kocha wa Yanga, Luc Eymael amesisitiza kwa uongozi kwamba si Molinga na Lamine pekee wanaopaswa kuadhibiwa kwa utovu wa nidhamu hata mastaa wengine, akiwemo Yondani,Mohammed Banka na Erick Kabamba nao wapewe siku tatu za kujieleza.

Endapo nyota hao watabainika kuwa na makosa, adhabu mbalimbali zinaweza kuwakumba ambazo ni kukatwa mishahara, kusimamishwa au kuondolewa kabisa ndani ya timu na tayari kocha ameuambia uongozi kwamba hatakuwa na Molinga msimu ujao.

Kabla ya mechi na Namungo, kocha huyo alizungumza kwa hasira kwamba amekerwa na kitendo cha baadhi ya wachezaji saba wa Yanga kujifanya mastaa kwa kuchagua mechi za kucheza huku akisisitiza kuwa kitendo hicho ni hujuma na kukosa nidhamu kwa timu pinzani.

Kocha huyo alisisitiza kwamba kuna wachezaji ambao waligoma kwenda Namungo kucheza huku wakicheza mechi za Dar es Salaam tu na mikoa ya jirani na akafoka kuwa; “Wanajiona wao ni Ronaldo au Messi...Hata Mane na Salah hawachagui mechi za kucheza. Ni kumkosea heshima mchezaji mwenzio.”

Kocha huyo aliwashtaki wachezaji hao kwa uongozi uwachukulie hatua na ndipo Molinga alipopewa barua ya kujieleza kwanini asichukuliwe hatua au kufukuzwa ndani ya siku 3. Lakini habari za ndani zinasema kocha aliposikia ni Molinga pekee akawajia juu viongozi kwa kushinikiza na wengine wapewe akiwataja kwa majina Yondani, Kabamba na Banka.

Habari za ndani ya Yanga zinasema kwamba juzi Jumatano, wachezaji hao walipewa barua zao za kujieleza ambapo siku ya tatu na ya mwisho ni leo Ijumaa.

“Kocha anasema Banka walipokuwa wanaenda kucheza na Singida alisema kajigonga goti kwenye gari, hivyo hawezi kucheza kaumia, Yondani naye siku timu inaondoka anajifanya ana matatizo ya kifamilia.

“Kabamba naye alidanganya anaumwa ili asiende mchezo na Namungo, Molinga naye eti mkewe kaja hivyo hawezi kusafiri,”kilifafanua chanzo chetu cha kuaminika ndani ya uongozi na kuongeza kwamba tayari walipokea barua ya Molinga lakini haina majibu ya kujitosheleza.

KOCHA ATETA

Mwanaspoti lilimtafuta Eymael ambaye alisisitiza hayuko tayari kuhusika kwenye hukumu za wachezaji hao kwani amesharipoti kwa uongozi wenyewe ndio wenye mamlaka ya mwisho.

“Mimi ni kocha nimeshatoa taarifa kwa uongozi na tayari waliomba vithibitisho na utetezi kutoka kwa wachezaji, najua Lamine Moro tayari ameshawasilisha utetezi wake.

“Ni jukumu la uongozi kupima na kufanya maamuzi ambayo wataoni ni sahihi kwasababu wao ndio waajiri na mimi pia ni mwajiriwa.

“Kuhusu Molinga bado sijapata taarifa zozote za utetezi na hilo ni jukumu lao,” alisema kocha huyo.