Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu Haaland kutumia majina tofauti timu ya Taifa

Muktasari:

  • Inaelezwa kuwa mshambuliaji huyo wa Norway aliomba kufanya hivyo kwenye jezi yake ya timu ya Taifa kama ishara ya kumuenzi mama yake na kutambua mchango wake katika kumkuza kisoka.

Bila shaka mashabiki wengi wa soka wamekuwa wakijiuliza kwa nini mshambuliaji wa Norway, Erling Haaland, hutumia jina la "Braut Haaland" kwenye jezi yake ya timu ya taifa, tofauti na "Haaland" pekee anapokuwa Manchester City.

Kwa mujibu wa utamaduni wa Norway, ni jambo la kawaida kwa mtu kubeba majina ya familia ya baba na mama. Hivyo, Haaland ameamua kuongeza jina la "Braut" ili kulitambulisha rasmi jina la familia ya mama yake katika ngazi ya kimataifa.

Hatua hiyo si ya bahati mbaya, bali ni uamuzi wa makusudi unaolenga kuenzi pande zote mbili za familia yake, hususan upande wa mama yake, Gry Marita Braut.

Mshambuliaji wa Norway, Erling Haaland. Picha na Mtandao

Mama yake, Gry Marita Braut, alikuwa mwanariadha mahiri na aliwahi kutwaa ubingwa wa taifa nchini Norway, huku akichangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya mtoto wake katika michezo.

Kwa miaka mingi, mshambuliaji huyo amekuwa akitumia jina la "Haaland" pekee katika klabu mbalimbali kutokana na sababu za utambulisho na umaarufu wa kibiashara uliotokana na baba yake, Alf-Inge Haaland, ambaye aliwahi kucheza katika Ligi Kuu England akizitumikia Leeds United na Manchester City.

Mshambuliaji wa Norway, Erling Haaland. Picha na Mtandao

Hata hivyo, Haaland ambaye ameifungia Norway, mabao 57 katika mechi 51 ameona ni wakati muafaka wa kuonyesha hadharani kuwa mafanikio yake yametokana na mchango wa wazazi wake wote wawili.

Kutokana na sababu hiyo, Haaland aliomba jina la "Braut Haaland" liwekwe kwenye jezi yake ya timu ya taifa, hatua inayotafsiriwa kama ishara ya kumuenzi mama yake na kutambua mchango wake katika kumkuza kisoka.

Kwa sasa, kila anapoiwakilisha Norway, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 huvaa jezi yenye jina "Braut Haaland", akionyesha kuthamini mchango wa wazazi wote wawili katika maendeleo yake ya soka.