Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yamal akataa kulinganishwa na Haaland, Mbappe

Muktasari:

  • Katika mchezo wa kwanza wa Hispania kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwaka huu dhidi ya Cape Verde, Yamal aliingia uwanjani akitokea benchi.

Nyota wa Hispania, Lamine Yamal amesema kwamba sio sahihi yeye kulinganishwa na Kylian Mbappe na Erling Haaland kwa vile wao wamemzidi umri.

Kauli hiyo ya Yamal imekuja kufuatia presha ambayo imeanza kuelekezwa kwake baada ya Mbappe na Haaland kuwa na mwanzo mzuri kwenye Fainali za Kombe la Dunia kulinganisha na yeye.

Ufaransa ilianza kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Senegal ambapo Mbappe alifunga mabao matatu huku Norway ikipata ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Iraq ambapo Haaland alipachika mabao mawili.

Hispania ilianza kwa kulazimishwa sare tasa na Cape Verde katika mchezo ambao Yamal alianzia benchi kwa kile kilichoonekana kwamba hakuwa fiti kiasi cha kutosha kuanza kwa vile ametoka kuuguza majeraha ya misuli.

Presha inaonekana imeanza kuelekezwa kwa nyota huyo wa Barcelona mwenye umri wa miaka 18 kwa kuonekana ameanza kwa kuzidiwa kete na Haaland na Mbape lakini mwenye amesema kuwa hastahili kuingizwa katika ulinganisho na wawili hao.

"Sihitaji hilo liwe jambo la kunivuruga kwa upande wangu. Sio suala la kumuiga Mbappe au kama Messi amefunga bao basi nihitaji kufunga moja pia. Hapana sijali kuhusu hilo.

"Wao wana miaka 10 kunizidi. Na pili staili yangu ya uchezaji ni tofauti. Ninataka kusikiliza. Ninaweza kufunga mabao 16 na baada ya hapo nikaishia nusu fainali. Kwa hiyo hicho sio ninachokitazama," amesema Yamal.

Licha ya kuwa na umri wa miaka 18, Yamal tayari amekuwa akitajwa kama miongoni mwa wachezaji bora duniani na ameshakuwa tegemeo katika timu ya taifa ya Hispania.

Mchezaji huyo alitoa mchango mkubwa katika kuiwezesha Hispania kutwaa ubingwa wa Kombe la Euro mwaka 2024.

Hispania itakabiliana na Saudi Arabia katika mchezo wa pili wa kundi lake na baada ya hapo itakamilisha kwa kucheza na Uruguay.