Kwa Mayele mtakula nyingi

Friday September 24 2021
mayeyapiccc
By Daudi Elibahati

KOCHA wa DTB FC, Ramadhan Nsanzurwimo amekiangalia kikosi cha Yanga na kuwaambia mashabiki wa timu hiyo watarajie makubwa kwa mshambuliaji wao mpya, Fiston Mayele kwani kwa jinsi alivyo wapinzani watakuwa wanakula nyingi sana uwanjani.

Kauli ya Nsanzurwimo inakuja baada ya kumshuhudia Mayele akiisaidia Yanga kuinyoosha chama lake kwa mabao 3-1 katika mchezo wa kirafiki, akimsifia aina ya uchezaji wake na kutahadharisha timu nyingine za Ligi Kuu Bara msimu huu inayoanza Jumatatu.

“Ni mchezaji msumbufu anayeweza kucheza kwa nafasi, unaweza usione madhara yake lakini anajua kucheza na akili za mabeki, hivyo naamini atawasaidia sana,” alisema kocha huyo wa zamani wa Singida United na Mbeya City.

Naye straika mpya wa DTB, Amissi Tambwe alisema ni suala la muda tu kwa Mayele ila anaamini akipata ushirikiano ataleta msaada mkubwa.

Advertisement